MAJAMBAZI WAVAMIA KITUO CHA POLISI KIMANZICHANA NA KUUA ASKARI.

Mnamo 11/06/14 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha ...

Mnamo 11/06/14 huko kituo kidogo cha Kimanzichana Pwani, watu wasiojulikana waliojifanya kuwa ni raia wema waliingia kituo kidogo cha Polisi Kiman nanzi Chana huku wakikimbia wakiwa na silaha za jadi kiasi cha askari wa zamu kuamini kuwa ni watu wanaohitaji msaada. 
Cha kushangaza watu hao walimvamia askari mwenye silaha ambaye amefahamika kwa jina la JOSEPH NGONYANI na kuanza kumkatakata mapanga na hatimaye kupora silaha SMG ikiwa na risasi 30. Ndipo walipoanza kushambulia kwa risasi askari wengine na kufanikiwa kupora SMG ya pili na risasi 30. Hatimaye watu hao wakapora risasi za akiba 41 na kutoweka kusikojulikana. 
Askari Ngonyani alifariki dunia alipokuwa anapatiwa matibabu kwenye hospitali wilaya ya Mkuranga. Askari mwingine aitwaye VENANCE amejeruhiwa mgongoni kwa risasi ambayo bado imo ndani, na kwenye paja la mguu wa kulia. Mgambo Mariam alijeruhiwa kichwani, shingoni na kuvimba bega kutokana na kupigwa sana mateke na kujeruhiwa mbavuni. 
Kwa mujibu wa mganga Mkuu wa zamu wa Hospitali hiyo aitwaye VERONICA MUSIME, anathibitisha askari huyo kufariki akiwa anapatiwa matibabu hapo Mkuranga wakati wengine wamekimbizwa Muhimbili kwa matibabu ya kina. Kazi ya Mungu haina makosa; vituoni tuwe makini sana na stahili hii ya ujambazi; HESHIMA PEKEE kwa marehemu na majeruhi hawa ni kuwapata watuhumiwa wote na silaha walizoiba bila kuchelewa. Bila kujali mkoa ulipo, taarifa za haraka tunatarajia kupata toka kwako kuhusiana na wahusika wa tukio hili. 
R.I.P Joseph Ngonyani

Related

MADIWANI MANISPAA YA MOSHI WASUSIA KIKAO CHA BAJETI

 Diwani wa kata ya Kaloleni ,Michael Mwita (CCM) akizungumza juu ya kitendo cha madiwani wenzake kutoka nje huku wakituhumu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo kuhusika katika uporaji wa viwanja v...

SPLM KUMALIZA MGOGORO SUDAN KUSINI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na viongozi wenzie  leo tarehe 22/01/2015  kabla ya kuanza kwa mkutano wa utiaji saini makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha...

MNUNUZI WA NYUMBA/KIWANJA HII NI NAMNA YA KITAALAM YA KUJUA ENEO UNALONUNUA KAMA LINA MGOGORO AU HAPANA

  Na   Bashir   Yakub Makala zilizopita  nilieleza   mambo au taarifa muhimu  zinazopaswa kuwa kwenye  mkataba wako  unapokuwa unanunua  nyumba/k...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904765
item