AJALI MBAYA YA FUSO SHINYANGA: WAWILI WAFARIKI, 29 WAJERUHIWA

  Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga   Hapa ni katika eneo la dharura katika hosp...

 Miili ya marehemu ikiwa katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa shinyanga
 Hapa ni katika eneo la dharura katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga ambapo majeruhi 29 hadi wamepokelewa kufuatia ajali ya gari aina ya fuso iliyokuwa imebeba watu wengi pamoja na mizigo kuelekea katika mnada wa Mhunze uliopo wilayani Kishapu mkoani Shinyanga. Ajali hiyo imetokea asubuhi ya leo Alhamis. Pichani majeruhi waliendelea kuhudumiwa na wataalam wa afya katika hospotali ya mkoa wa Shinyanga
 Kwa mujibu wa kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel ameiambia malunde1 blog kuwa mpaka sasa wamepokea miili miwili ya marehemu na majeruhi 29

 Baadhi ya majeruhi wameiambia malunde1 blog kuwa gari aina ya fuso waliyokuwa wamepanda tena kwa kujazana ilikuwa inafukuzana na fuso nyingine na ghafla walijikuta wakiwa wameshapinduka
 Kulia ni kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akichukua maelezo kutoka kwa askari wa usalama barabarani
 Majeruhi akipelekwa wodini
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Shinyanga Dkt Maguja Daniel akizungumza na waandishi wa habari hivi punde

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Related

OTHER NEWS 5228669575168627315

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item