CAG AMUITA KAFULILA KUTOA USHAHIDI SAKATA LA IPTL

  Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh MOROGORO.  Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) amemua...

 Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh

MOROGORO.
 Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) amemuandikia barua mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila akimtaka kufika ofisi za taasisi hiyo Julai 23 mwaka huu, akiwa na ushahidi wote kuhusu tuhuma za ufisadi wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL).
Kafulila aliibua kashfa hiyo wakati wa Bunge la Bajeti alipodai kuwa Sh200 bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya escrow, ambayo ilifunguliwa kuweka fedha wakati mgogoro baina ya IPTL na Shirika la Umeme (Tanesco) ukiwa mahakamani kusubiri kutolewa uamuzi, zilichotwa kifisadi na kutaka Bunge liunde kamati huru kuchunguza.
Hata hivyo, Bunge lilimuagiza CAG na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza tuhuma hizo za uchotaji wa fedha hizo.
Jana CAG Ludovick Utouh alisema kuwa wamemwandikia barua mbunge huyo wakimtaka aende kutoa ushahidi kuhusu sakata hilo, huku akisisitiza kuwa Kafulila siyo mtu wa kwanza kuhojiwa na ofisi yake kuhusu suala la IPTL.
“Lengo letu ni kukusanya ushahidi wote na kusikiliza watu wanaojua kuhusu IPTL ili tuweze kujua ukweli wa hili jambo,” alisema Utouh.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kafulila alisema kuwa amepewa ujumbe kutoka ofisi hiyo jana mchana na kuelezwa kuwa barua yake ya kuitwa kutoa ushahidi huo ametumiwa kupitia sanduku lake la Posta.
Kuitwa kwa Kafulila na CAG kumekuja ikiwa zimepita siku tatu tangu IPTL ilipomfungulia mashtaka mbunge huyo dhidi ya tuhuma alizozitoa za wizi wa pesa kwenye Akaunti ya Tegeta Escrow iliyoko Benki Kuu (BoT).
Kafulila amefunguliwa kesi ya madai Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam na IPTL kwa kushirikiana na kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (mlalamikaji wa pili) na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hizo, Harbinder Sigh Seth (mlalamikaji wa tatu), Julai 13 mwaka huu.
Katika kesi hiyo namba 131 ya mwaka 2014, walalamikaji kwa pamoja wanaiomba mahakama imwamuru mbunge huyo awalipe fidia ya jumla ya Sh310 bilioni kwa madai ya kutoa kashfa dhidi yao kwa kuwatuhumu kujipatia pesa kwa njia zisizo halali.
“Ofisi ya CAG wameniita na nimewakubalia. Kikubwa nitawaeleza kwanza namna ambavyo mchakato mzima wa PAP kumiliki IPTL ulivyoambatana na uvunjifu wa sheria ya fedha (Finance Act 2012.sec29),” alisema.
Kafulila alisema jambo jingine atakalowaeleza ni jinsi ambavyo makubaliano ya kutoa fedha hizo yalivyokuwa na nia ovu kwani sehemu ya makubaliano hayo yanasomeka kwamba mchakato huo uwe siri baina ya pande mbili kwa maana ya IPTL na PAP (ambayo iliinunua IPTL).
“Pia kwa upande mmoja na Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco) na IPTL kwa upande wa pili. Hoja ya kujiuliza ni kwanini kipengele cha siri kama utoaji fedha hizo haukuwa uamuzi ovu?” alihoji.

Kwa mujibu wa sheria za akaunti ya escrow, fedha zinazowekwa hutakiwa kutoka kwa idhini ya pande zote mbili kwa ajili ya malipo ambayo ni lazima yafanywe wakati kesi ikiendelea na iwapo kesi itamalizika, fedha hizo zitalipwa kwa mujibu wa hukumu.

Zaidi ya Sh400 bilioni zilikuwa zimewekwa kwenye akaunti hiyo wakati kukiwa kuna mgogoro wa kisheria baini ya wabia wa zamani wa IPTL (VIP Engeneering and Marketing na Mechmar Corporation ya Malaysia) kwa upande mmoja, Tanesco na IPTL kwa upande mwingine, lakini baada ya kikao cha pamoja baina ya wabia hao, Tanesco na Wizara ya Madini, zaidi ya Sh200 bilioni zilitolewa na PAC ikalipwa.

 MWANANCHI

Related

OTHER NEWS 1618636197957591208

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item