TAIFA STARS KUPIGA KAMBI MBEYA KUJIANDAA NA MSUMBIJI
Kikosi cha Taifa Stars kitapiga kambi ya wiki moja kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji. Mechi hiyo ya raundi ya pili y...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/07/taifa-stars-kupiga-kambi-mbeya.html
Kikosi cha Taifa Stars kitapiga kambi ya wiki moja
kujiandaa kwa mechi ya marudiano dhidi ya Msumbiji.
Mechi hiyo ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika kutafuta tiketi ya kushiriki Fainali za Afrika (AFCON) zitakazochezwa mwakani nchini Morocco itafanyika wikiendi ya Agosti 2 na 3 mwaka huu nchini Msumbiji.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager itaondoka nchini Julai 31 mwaka huu kwenda Johannesburg, Afrika Kusini ambapo itafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kutua Maputo kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto.

MECHI YAINGIZA SHILINGI MILIONI 158
Mechi ya michuano ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Msumbiji (Mambas) iliyochezwa juzi (Julai 20 mwaka huu) imeingiza sh. 158,350,000 kutokana na washabiki 19,684 walioingia kwa kiingilio cha sh. 7,000 na sh. 30,000.
Mgawo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) sh. 24,155,084.75, gharama za tiketi (MaxMalipo) sh. 19,684,000, gharama za mchezo sh. 22,902,183, uwanja sh. 11,451,092, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 5,725,546 na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 74,432,095.
Tunawashukuru washabiki wote waliojitokeza kwenye Uwanja wa Taifa kuishangilia Taifa Stars katika mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 2-2.
MUDA WA USAJILI WAONGEZWA KWA WIKI MBILI
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeongeza muda wa usajili kwa wiki mbili ili kuzipa klabu nafasi ya kukamilisha taratibu zinazotakiwa. Hivyo hatua ya kwanza ya usajili inakamilika Agosti 17 mwaka huu badala ya Agosti 3 ya awali.
Kutokana na marekebisho hayo, kipindi cha uhamisho kinakamilika Agosti 17 mwaka huu wakati pingamizi itakuwa kati ya Agosti 19 hadi 26 mwaka huu.
Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji itathibitisha usajili kati ya Septemba 1 na 2 mwaka huu.
Uhamisho wa kimataifa, usajili wa wachezaji huru, na utatuzi wa dosari za usajili unatakiwa uwe umekamilika kufikia Septemba 7 mwaka huu. Uthibitisho wa hatua ya mwisho ya usajili utafanywa Septemba 15 mwaka huu.
Kwa upande wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu wa 2014/2015 itaanza Septemba 20 mwaka huu, na ratiba itatolewa mwezi mmoja kabla ya kuanza ligi hiyo.