DC MPANDA-KATAVI AAGIZA WANAFUNZI WALIOKATISHA MASOMO KURUDI SHULE

  Na Kibada Kibada–Mpanda  Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda na H...

 
Na Kibada Kibada–Mpanda 
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda pamoja na Kamati ya ulinzi na usalama kuhakikisha wanatekeleza maagizo yaliyotolewa na kikao cha ushauri wilaya ya kufanya operation ya wanafunzi watoro walioacha shule na kuhakikisha wanarudi kuendelea na masomo ya sekondari.
 
Mkuu wa Wilaya huyo aliagiza mwezi juni wakati shule zimefungwa kuhakikisha wanafunzi wote waliokatisha masomo kwa sababu mbalimbali kama mimba, utoro wa kawaida au kujifungua wanarudi shuleni kuendelea na masomo, lakini inaonekana agizo hilo halijafanyiwa kazi.
 
Tatizo la utoro kwa shule nyingi za Msingi na Sekondari Wilayani Mpanda linaonekana kushika kasi hali iliyomfanya Mkuu wa Wilaya kuagiza wanafunzi waliokatiza masomo warudi shuleni .
 
Akizungumza katika mikutano yake ya hadhara na wananchi wa wilaya hiyo katika ziara zake za kuhimiza maendeleo wilayani humo pamoja na vikao vya wazazi,walimu na wadau wa elimu katika shule ya sekondari Mpanda ndogo alipokea taarifa ya masikitiko ya utoro katika shule hiyo .
 
Kufuatia taarifa hizo aliagiza wakurugunzi wote wilayani , wazazi, kusaidiana na watendaji wa serikali na kamati za shule kuhakikisha wanafunzi wote wanarudi shuleni.
Katika kikao hicho pia aliagiza kuhakikisha wanakamilisha ujenzi wa maabala kwa shule zote za sekondari wilayani humo.

Related

ELIMU 5092524677503589185

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item