MAAMBUKIZI YA UKIMWI NCHINI YAPUNGUA KWA ASILIMIA 33
Na Rose Masaka na Lorietha Laurence-MAELEZO TANZANIA ni miongoni mwa Nchi ambazo zimeweza kupunguza maambuzi ya ugonjwa wa Uki...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/08/maambukizi-ya-ukimwi-nchini-yapungua.html
Na Rose Masaka na Lorietha Laurence-MAELEZO
TANZANIA ni miongoni mwa Nchi ambazo zimeweza kupunguza maambuzi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa asilimia 33.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu Mhe. William Lukuvi wakati akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu
Mkutano wa 20 wa Kimataifa wa Ukimwi Duniani uliofanyika Melbourne
nchini Australia Julai mwaka huu.
Amesema
kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya Serikali kuanza zoezi la kuzuia
maambukizi kutoka kwa mama mjamzito kwenda kwa mtoto, na tohari kwa
wanaume hasa kwa jamii iliyokuwa haifanyi hivyo.“Tohari
zinaonyesha kwa wanaume inapunguza maambukizi kwa asilimia 60 na
wanawake asilimia 44. Tiba ya UKIMWI kwa mama mwenye virusi vya UKIMWI
inapunguza maambukizi mapya kwa mtoto kwa asilimia 97 na tiba kwa watu
wazima wa kawaida inapunguza maambukizi mapya kwa asilimia 96,” amesema
Lukuvi.
Naye
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania Dkt. Fatma
Mrisho amesema kuwa sababu zinazochangia maambukizi mapya ni pamoja na
baadhi ya mila desturi potofu za kitanzania ,ikiwemo ndoa za utotoni,
kurithi wajane, wanaume kuwa na wanawake wengi na kuogopa kupima afya.Mkutano
huo ulikuwa na kauli mbiu iliyosema “Ongeza hatua katika juhudi zote za
kuthibiti Ukimwi” ulisisitiza mapambano dhidi ya Ukimwi yanahitaji njia
mbalimbali ikiwemo ushiriki wa wadau na umuhimu wa kutenga fedha kwa
ajili ya shughuli za Ukimwi kutoka vyanzo vya ndani ya nchi na taasisi.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wajumbe 11,200 kutoka katika nchi 146 ikiwemo Tanzania.