JESHI LA POLISI LAMJIBU MBOWE,HAKUNA MAANDAMANO WALA MIGOMO
Na Karoli Vinsent SIKU moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,kutang...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/09/jeshi-la-polisi-lamjibu-mbowehakuna.html
Na Karoli Vinsent
SIKU moja kupita baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe,kutangaza mgomo na Maandamano nchi nzima kwa ajili ya kushinikiza Bunge la Katiba lisitishwe mara moja kwa madai Bunge hilo limeshindwa kutengeneza katiba ya Nchi, badala yake linatunga Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM, Naye Mkuu wa jeshi la polisi Nchini IGP Ernest Mangu ameibuka na Kumvaa Mwenyekiti huyo wa Chadema Freeman Mbowe na kusema Jeshi hilo halitakubali kuona amani ya nchi inavurugwa.
Kwani Maandamano hayo pamoja na migomo ni kinyume cha sheria na kanuni zinazosimamia Jamii kutii sheria na utaratibu wake.
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam Kamishina wa polisi Oparesheni na Mafunzo Paul Chagonja -CP kwa Niaba ya Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Ernest Mangu wakati wa Mkutano na Waandishi wa habari kuzungumzia kauli aliyoitoa Kiongozi huyo wa Chadema,ambapo Chagonja alisema Jeshi hilo halitakubali kushuhudia Migomo na Maandamo yenye kulenga kuvuruga Amani
“Jeshi la polisi tumepokea kwa masikitiko makubwa kauli aliyoitoa Freeman Mbowe kwamba yeye pamoja na wafuasi wake wa chama chake wanajipanga kufanya maandamano na migomo isiyokomo nchi nzima bila kufuata sheria,kanuni na taratibu za nchi ili kushinikiza Bunge la katiba kuhailishwa ,sisi jeshi la polisi tunaonya vikali kauli hiyo ambayo ni kinyume cha taratibu za nchi na hatutakubali”alisema CP-Chagonja
Chagonja alizidi kusema ieleweke wazi kwamba siasa zina mipaka na zinapovuka mipaka hiyo na kuanza kwenda kinyume cha sheria,kanuni na taratibu za nchi hiyo inageuka kuwa jinai na wala siyo siasa tena.
Aidha Chagonja alisema Jeshi hilo la polisi aliweza kumvumilia mtu yeyote atakayetumia mwavuri wa siasa kutaka kuvuruga Amani na utulivu uliopo hapa nchini na Jeshi halitasita kumchukulia hatua kali kama mhalifu Mwengine yeyote.
Katika hatua nyingine Jeshi la polis limewataka wananchi wote kufuata sheria na taratibu za nchi na kuepuka kauli zenye kulenga kuvuruga Amani ya nchi.
Kauli hiyo ya Jeshi la Polisi nchini limekuja siku moja baada ya Mwenyekiti waChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),Freeman Mbowe kutangaza kuwepo kwa maandamano bila kikomo nchi nzima kushinikiza kusitishwa kwa Bunge la Katiba aliloliita la kifisadi linaloendelea mjini Dodoma.
Pia, Chama chake kimeazimia kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais ifikapo mwakani, lengo likiwa kuung’oa utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliowafanya watanzania kuwa maskini wa kutupwa.
Akihutubia mkutano mkuu wa uchaguzi, Mwenyekiti huyo wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe, alisema umefika wakati sasa wa kuacha kukaa na kuzungumza na kwani kinachoendelea Dodoma ni wizi na ukatili wa hali ya juu kwa wananchi wanyonge ambao ndio walipa kodi.
“Samahani maneno yangu ni makali na wala hapa sifanyi uchochezi…kinachoendelea Dodoma ni ufisadi na wizi, tumekaa Kinana, tumekaa na Mangula, tumekaa na Rais Kikwete tumekubaliana bunge lisitishwe lakini wanamwacha Sita afanye anachotaka kama utafikiri ndiye Rais…
“Anachakachua rasimu, anabadili kanuni, anavunja sheria anakusanya maoni utafikiri yeye ni Warioba…hiki hakivumiliki, naomba mkutano huu utoke na tamko,” alisema Mbowe na kushangiliwa na wajumbe wakiafiki.
Mbowe akipendekeza maadhimio, alisema kinachotakiwa ni kuungana na kufanya maamuzi ya kuandamana nchi nzima kushinikiza kusimamishwa kwa Bunge la Katiba linaloendelea mjini Dodoma ambalo linafuja fedha za wanyonge ili hali katiba haitapatikana