BUNGE LA KATIBA: SAMWEL SITTA ATANGAZA RATIBA YA UPATIKANAJI WA KATIBA
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amesoma ratiba kamili ya mchakato wa katiba mbele ya wajumbe ili kuhakikisha ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/09/bunge-la-katiba-samwel-sitta-atangaza.html
MWENYEKITI wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta amesoma ratiba kamili ya mchakato wa katiba mbele ya wajumbe ili kuhakikisha kuwa malengo ya upatikanaji wa katiba hiyo yanafikiwa.
Aidha, siku ya tarehe 21 Jumamosi, Kamati ya Uongozi itaketi ili kuona namna ilivyokaa Rasimu ya mwisho, ambapo tarehe 22 siku ya Jumatatu, Kamati ya Uandishi itawasilisha bungeni hapo Rasimu hiyo kwa muda wa Nusu siku ambapo wajumbe watapewa muda wa kuitafakari rasimu hiyo siku ya Jumatatu na Jumanne.
“Siku ya tarehe 24 na 25 yaani Jumatano na Alhamisi, Wajumbe wa bunge hilo watakuwepo bungeni hapo kwa muda wa siku zote mbili kwa lengo ya kufanya kazi ya kuhakiki na sio kufungua upya mjadala, uhakiki huo unamaanisha kupata kujua juu ya yale waliyokubaliana kama kweli yamo kisha badala ya uhakiki huo, watarejesha kwa kamati ya uandishi ili ifikapo siku ya tarehe 26 kamati hiyo iweze kufanya kazi ya kurekebisha kulingana na yale wajumbe watakayowaambia kamati hiyo”, alisema Mhe. Sitta.
Kura zitaanza kupigwa siku ya Jumatatu ya tarehe 29 saa tatu asubuhi kwa kuanza na Ibara ya kwanza mpaka ya mwisho pasipo kubadilishwa badilishwa ambapo zoezi hilo linatazamiwa kumalizika kati ya tarehe mbili au tatu asubuhi.
Imeandikwa na Benedict Liwenga, Dodoma/Tanzania Government Blog