TANZANIA KUUNGANA NA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUADHIMISHA SIKU YA KIMATAIFA YA HIFADHI YA TABAKA LA OZONI.
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhi...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/09/tanzania-kuungana-na-jumuiya-ya.html
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Mhe. Mhandisi Dkt. Binilith Mahenge akiongea na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni linalofanyika leo 16 Septemba, 2014.
DODOMA
Tarehe 16 Septemba, mwaka huu Tanzania inaungana na Jumuiya ya Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Hifadhi ya Tabaka la Ozoni kama ilivyoagizwa na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika azimio lake la 49/114 la tarehe 19 Desemba, 1994.
Hayo yamesemwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Mhe. Mwandisi Dkt. Binilith Mahenge wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari 15 Septemba, 2014 kwa lengo la kuongelea juu ya Maadhimisho hayo yanayofanyika leo tarehe 16 Septemba mwaka huu.
Mawiri Mahenge ameeleza kuwa tarehe hiyo ni kumbukumbu ya kutiwa saini Mkataba wa Montreal (Montreal Protocol-1987) kuhusu kemikali zinazomonyoa Tabaka la Ozoni kwa kudhibiti utengenezaji na matumizi ya kemikali zinazoharibu Tabaka hilo.
Ameendelea kwa kusema kuwa Mkataba huo umepata mafanikio makubwa ya kupunguza zaidi ya asilimia 98% ambapo ni takribani tani milioni 1.8 ya uzalishaji na matumizi ya kemikali zinazomong’onyoa Tabaka la Hewa ya Ozoni.
“Punguzo hilo limechangia katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwasababu baadhi ya kemikali zinamong’onyoa tabaka la ozoni pia husababisha kuongezeka kwa joto duniani”, alisema Dkt. Mahenge.