MOTO WAUNGUZA MADUKA YA VIPODOZI MWENGE

Baadhi ya wafanyabiashara eneo la Mwenge stendi ya daladala wakijaribu kuokoa mali zao baada ya maduka yao kuungua moto.                    ...




Baadhi ya wafanyabiashara eneo la Mwenge stendi ya daladala wakijaribu kuokoa mali zao baada ya maduka yao kuungua moto.



                                                     Wananchi wakishuhudia tukio hilo.

                                           Baadhi ya maduka ya vipodozi yakiungua moto.


 Askari wa Kikosi cha Zima moto akizima moto huo uliokuwa ukiunguza maduka ya vipodozi.

MADUKA kadhaa ya vipodozi, nguo yameungua moto na kusababisha hasara kubwa kwa wamiliki wake.
Moto huo umetokea mishale ya saa 5.20 leo asubuhi baada ya kutokea hitilafu ya umeme kwenye moja ya kibanda cha biashara.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, moto huo ulianza taratibu kisha kupamba moto.
Wafanyabiashara wa maduka ya vipodozi ndiyo waliopata hasara kubwa kwa mali zao kuharibika kufuatia kutaka kuziokoa.
Hata hivyo, Kikosi cha Zima moto kilichofika eneo la tukio kwa wakati na kimepongezwa kwa kufanya kazi nzuri na kuweza kuudhibiti moto huo.
Adha, jeshi la polisi limepongezwa kwa kazi nzuri lililoifanya ya kudhibiti vibaka ambao walijiandaa kufanya uhalifu wa kuiba mali katika kurupushani hizo za uokoaji.

Source: Global Publishers

Related

OTHER NEWS 5766567673746117162

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item