ALIYEMILIKI JENGO LILILOPOROMOKA AKAMATWA

Jeshi la Bangladesh linajitayarisha kutumia zana nzito kuondosha kifusi katika jengo la viwanda liloporomoka Jumatano na kuuwa mamia ya wat...

Jeshi la Bangladesh linajitayarisha kutumia zana nzito kuondosha kifusi katika jengo la viwanda liloporomoka Jumatano na kuuwa mamia ya watu.

Wafanya kazi za uokozi wanatoboa shimo kwenye kifusi kujaribu kuwafikia haraka manusura walionasa wakati jengo hilo lilipoanguka.
Baadhi ya waokozi wameondolewa kwa sababu hawakuweza kuhimili uvundo mkali wa maiti zilizooza ndani ya kifusi.
Watu 2400 wamenusuriwa tangu jengo hilo la ghorofa nane kuporomoka mjini Dhaka.
Zaidi ya watu 360 wanajulikana kuwa wamekufa.
Msemaji wa jeshi la Bangladesh, Brigadier General Siddiqul Alam Sikder, alisema hawataondoa kifusi kwa sasa, ila katika kusaidia kumuokoa mtu:
"Hatutaondoa chochote hadi tuna hakika kwamba hakuna mtu aliye bado hai ndani ya kifusi.
Makundi yote yanayofanya uokozi chini ya kifusi yatatuarifu.
Tukipata taarifa hiyo, tutakutana kuamua kama tutaingia kwenye kifusi, au tunyanyue paa kwa crane.
Kisha tutaingia kipindi cha pili cha operesheni."

SOURCE: BBC Swahili

Related

OTHER NEWS 305964049754738265

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

item