WANAWAKE KWENYE MIEREKA TUPO, HII NI KUTOKA SENEGAL
Nchini Senegal, miereka ya kitamaduni inapendwa zaidi kuliko soka huku wachezaji wakijipatia pesa nyingi na hata kuwa watu maarufu. Kat...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/04/wanawake-kwenye-miereka-tupo-hii-ni.html
|
Nchini Senegal, miereka ya kitamaduni inapendwa zaidi kuliko soka huku wachezaji wakijipatia pesa nyingi na hata kuwa watu maarufu. Katika sehemu nyingi za nchi mchezo huu ni wa wanaume pekee lakini katika maeneo ya mashinani , hususan Kusini mwa nchi ya senegal, kuna historia ndefu ya wanawake kushiriki miereka na ndio maana timu ya taifa inajumuisha watu kutoka eneo hilo.
|
|
Wanawake hawa hufanya mazoezi mara kadhaa kwa wiki katika ufukwe wa bahari. Miereka ya kitamaduni inatofautiana kidogo na miereka ya Olimpiki na wanawake hujifunza mbinu tofauti ili kuweza kushindana. Mwana miereka mashuhuri zaidi mwanamke nchini Senegal , Isabelle Sambou, anatoka eneo la Casamance. Alishiriki michezo ya olimpiki mwaka jana na akaweza kuwa katika nafasi ya tano.
|
|
Sirefina Diediou alijiunga na kikosi cha taifa mwaka jana. Anasema likuwa anapigana na vijana alipokuwa shuleni na ilimchukua mamake muda kukubali kuwa anapenda mchezo huu. |
|
Miereka huambatana na densi za kitamaduni. Katika sherehe za hivi karibuni katika kijiji cha Diembering,wanamiereka wanaume wanajipanga kushiriki densi ya kitamaduni wakati wa kufungua rasmi shindano la miereka. |
|
Wasichana wadogo pia walishiriki miereka kujifurahisha tu kwa sababu kulikuwa na zawadi kama baiskeli, saa na komputa za kushindaniwa |
|
Kuvutana nywele hairuhusiwi wakati wa miereka lakini refarii haonekani kama anawatizama wawili hawa. |
|
Wasichana wanapaswa kuvua mikufu yao lakini baadhi yao wanapuuza sheria |
|
Wasichana wengi huwa hawashiriki miereka kwa sababu ya kwenda shule au katika vyuo vikuu na wengine kwa sababu ya mimba za mapema |
|
Mengi ya mavazi wanayovalia wanaume huwa ina maana yake, wanaume hawa hata hivyo wamevalia mavazi haya ili kuwaletea bahati njema waweze kushinda |
|
Densi hii inapaswa kuonyesha wanaume walivyo wakakamavu tayari kwa miereka |
|
Wanaume ambao hawawezi kushiriki miereka, huvalia kama wanawake, na kuwachangamsha mashabiki. Edouard aliye kushoto ni mfanyakazi katika moja ya makampuni katika eneo hilo hakuweza kushiriki miereka kwa sababu amejiumiza mguu. Licha ya hilo alikuwepo kwenye sherehe hizo. |
|
Zamani mchezo huu haukuwa na refari kwani mashabiki ndio wangeamua mshindi lakini siku hizi mambo yamebadilika kwani marefa ndio wanaamua mshindi |