WAZIRI MKUU WA ZAMANI WA ITALIA BERLUSCON AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 7 JELA

Waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi kushoto na kulia ni Karima El Mahroug ITALY: Jopo la majaji limemuhukumu waziri mkuu wa za...

Waziri mkuu wa zamani wa Italia Silvio Berlusconi kushoto na kulia ni Karima El Mahroug

ITALY:
Jopo la majaji limemuhukumu waziri mkuu wa zamani Silvio Berlusconi kifungo cha miaka saba (7) jela kwa kosa la kufanya mapenzi na binti wa miaka 17 aitwaye Karima el Mahroug aliyekuwa anajishughulisha na biashara ya kuuza mwili wake.

Hata hivyo wakili wa mshitakiwa Nicole Ghedini amepanga kukata rufaa hukumu hiyo kutokana na mtuhumiwa kutotendewa haki kwenye kesi hiyo, alikaririwa "What happened today is very serious,"huku akisisitiza kuwa majaji hawakutenda haki kwa mteja wake. Berlusconi, 76 alikana mashitaka yote likiwemo lile la May 2010 ambapo alishinikiza kuachiwa huru kwa binti huyo Karima alipokuwa amefungwa jela kwa kosa la wizi.

Wakati huohuo El Mahroug alikana kuwahi kufanya mapenzi na Berlusconi na kusema kuwa alimdanganya umri waziri huyo kuwa ana miaka 24.

Related

OTHER NEWS 7868360459966590003

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item