CUF: MAANDAMANO YAPO PALEPALE

Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro. Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema maandamano ambayo awali kilipanga kufanya...


Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro.

Chama Cha Wananchi (CUF), kimesema maandamano ambayo awali kilipanga kufanya Juni 29, mwaka huu kuelekea Ikulu lakini yakaahirishwa kutokana na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama yako pale pale.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema kwa sasa viongozi wengi wa chama wapo mikoani, lakini watakaporudi jijini Dar es Salaam chama kitafan

ya mkutano utakaopanga lini maandamano hayo yafanyike.
“Hatujakutana bado. Wajumbe wengi tupo mikoani. Sasa tutakaporejea Dar es Salaam tutapanga siku ya kukutana. Halafu tutapanga siku ya maandamano na  tutawajulisha,” alisema Mtatiro.

Kwa mujibu wa CUF, maandamano hayo yana lengo la kumfikishia ujumbe Rais Jakaya Kikwete, kwa kile wanachodai kuwa vitendo vya ukatili, wizi, ubakaji na mauaji vinavyofanywa na polisi mkoani Mtwara na kutaka uchunguzi kuhusu matukio ya Arusha.

Hata hivyo, kuahirishwa kwa maandamano hayo kulikuja baada ya Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuyapiga marufuku na kuonya kwamba polisi wangepambana na yeyote ambaye angekaidi amri hiyo.  

SOURCE: NIPASHE

Related

BARABARA ZITAKATOFUNGWA SIKU YA JUMANNE KUPISHA MSAFARA WA OBAMA NI HIZI

Sam Nujoma RoadSiku ya jumanne tarehe 02/07/2013 barabara zifuatazo hazitakuwa hewani (zitafungwa) kwa muda wa masaa 2 kuanzia saa 3.00 asubuhi:ALI HASSAN MWINYISAM NUJOMAMOROGORO

FBI KUCHUJA VIONGOZI WATAKAO MPOKEA NA KUONANA NA OBAMA

Dar es Salaam. Wakati magari 150 ya msafara wa ziara ya Rais Barack Obama yamewasili nchini, majina ya mawaziri wa Tanzania yatakayoruhusiwa kumpokea kiongozi huyo kuchujwa na makachero wa FBI. Mkur...

OBAMA ATOA SABABU ZILIZOMFANYA ASIENDE KENYA KWA SASA... SABABU KUBWA NI KESI YA UHURU KENYATTA NA MAKAMU WAKE

US President Barack Obama said Saturday the “timing was not right” for him to travel to Kenya, his father’s homeland, during his current Africa tour, but he expected to go there many times in the f...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904746
item