TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA 2014 KUANZA KUUZWA TAREHE 20 AUGUST, 2013 ANGALIA BEI ZAKE HAPA

Mauzo ya tiketi ya kombe la dunia yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira wa miguu yataanza kuuzwa rasimi Agusti 20 mwaka...


Mauzo ya tiketi ya kombe la dunia yaliyokuwa yakisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa mpira wa miguu yataanza kuuzwa rasimi Agusti 20 mwaka huu, FIFA imetangaza rasmi.

Bei za tiketi kwa ajili ya mashabiki wa kutoka nje ya Brazil watakaokwenda nchini Brazil kuangalia fainali za kombe la dunia zitaanzia bei ya $90 (£59, 69 euros) kwa mechi za makundi.
FIFA imetangaza kwamba tiketi ya bei rahisi kabisa kwa mashabiki wataokwenda Brazil kwa ajili ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo itaanzia $440 (£288) na ya bei ghali kabisa itakuwa kiasi cha  $990 (£650) ambayo ni sawa na 1,603,800 kwa fedha za kitanzania.

Michuano hiyo itaanza  tarehe 12 June, 2014 na mechi ya kwanza ya ufunguzi ikichezwa jijini Sao Paulo.

Tiketi zitaanza kuuzwa tarehe 20 August, 2013. Mashabiki wana muda mpaka 10 October kutuma maombi ya kununua tiketi na utafanyika uchaguzi wa kuamua maombi yapi yamepita.


Kuna jumla ya tiketi millioni 3 ambazo zipo kwa ajili ya maombi ya manunuzi ya mashabiki. 


BEI ZA TIKETI ZA KOMBE LA DUNIA (MASHABIKI NJE YA BRAZIL)

Matches Category 1 Category 2 Category 3

Opening Match $495 $330 $220
Group Matches $175 $135 $90
Round of 16 $220 $165 $110
Quarter Finals $330 $220 $165
Semi Finals $660 $440 $275
3rd / 4th Place Match $330 $220 $165
Final $990 $660 $440

Kwa raia ya wa Brazil tiketi ya bei rahisi kabisa itaanzia kwenye kiasi cha $15. Hizi zinapatikana kwa wanafunzi tu, na wale watu wenye umri zaidi ya miaka 60 ambao wapo kwenye mipango ya kusaidia jamiii. Kwa wabrazil wengine wote bei ya chini kabisa itaanzia kiasi cha $30. 

Bei ya chini kabisa ya tiketi katika michuano ya kombe la dunia mwaka 2010 nchini South Africa ilikuwa ni  $20, na pia ilikuwa kwenye mechi za  makundi.
FIFA mwanzoni ilisema kwamba tiketi za kombe la dunia mwaka 2014 zitakuwa za bei rahisi kuliko zote.

Katika mtandao rasmi wa kuuza tiketi wa FIFA kutakuwepo na ramani ya ya uwanja inayokuonyesha sehemu za kukaa kutokana na bei ya tiketi yako.
Hi inamaanisha kwamba hakutakuwa na kuhangaika katika kujua ni wapi unapaswa kukaa, alisema mkurugenzi wa masoko wa FIFA  Thierry Weil, ambaye ndio anayehusika na masuala ya yote tiketi.

Mashabiki wanaweza kuomba angalau siti nne kwa mechi, na kwa mechi saba tu. Amesema pia kutakuwa na mfumo wa kuuza tena tiketi ikiwa watu waliomba au kununua tiketi kabisa na wakashindwa kufika uwanjani. 
Angalau tiketi 400,000 zitawekwa maalum kwa mashabiki wa nchi mwenyeji, huku karibia tiketi 50,000 zikiwa maalum kwa ajili ya wajenzi wanaojenga viwanja vitakavyotumika kwenye michuano hiyo.

KWA WATANZANIA MNAOTAKA KUOMBA KUNUNUA TIKETI UNAWEZA KUINGIA KWENYE MTANDAO HUU - www.ticket.org/WorldCup

Related

KINANA AHUTUBIA MKUTANO MKUBWA TANGA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano wa hadhara ulioandaliwa maalumu kwa ajili ya kuwapongeza wananchi kuwachagua viongozi wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali ...

IPTL YASHUSHA BEI YA UMEME KWA ASILIMIA 20

KAMPUNI ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) ikiwa chini ya uongozi wa kampuni ya Pan African Power Solutions (T) Limited (PAP) imetangaza kufikia kwa punguzo la bei y...

NYALANDU ATANGAZA RASMI KUWANIA URAIS 2015

  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazalo Nyalandu alisalimia wananachi baada ya kuwasili na mkewe Faraja Kota kwenye Mkutano wa jimbo uliofanyika kwenye Uwanja ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904765
item