CUF WAJIPANGA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA JWTZ, POLICE

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kinawasilisha na mawakili wake na asasi za haki za binadamu kujua hatua za kisheria kuchukua dhidi ya  a...


CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kinawasilisha na mawakili wake na asasi za haki za binadamu kujua hatua za kisheria kuchukua dhidi ya  askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa madai ya kutekwa na kuteswa Naibu Mkurugenzi wa CUF Taifa, Shaweji Mketo, na viongozi wengine wa chama hicho Mkoa wa Mtwara.
Mpango huo ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wake wa Taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba wakati akiongea na waandishi wa habari.

Prof. Lipumba alisema pia chama hicho kinawasiliana na mawakili hao kujua hatua za kisheria za kuch

ukua dhidi ya Jeshi la Polisi kwa madai ya kuwabambikia kesi viongozi hao  ambao kimedai walikamatwa na kupigwa na askari wa JWTZ katika kambi yao ya Naliendele.
Alisema pia wanawasiliana na asasi za kiraia zinazoshughulikia haki za binadamu na haki za wanawake kumsaidia kisaikolojia mwanamke anayedaiwa kubakwa na askari wa JWTZ mkoani humo na kufikishwa mahakamani.

Lipumba aliwataja viongozi wengine wa CUF waliodaiwa kutekwa na kuteswa kambini Juni 28, mwaka huu kuwa ni Salum Mohamed ambaye ni Mwenyekiti wa CUF Mtwara Mjini,Ismail Jamal Mwenyekiti wa CUF Mtwara vijijini.

Wengine ni Mwenyekiti wa Vijana Mtwara mjini, Ismail Njalu, Katibu wa CUF Mtwara mjini, Said Kulaga na Kashindye Kalungwana ambaye ni dereva wa jeshi hilo makao makuu.

Alidai viongozi hao baada ya kutekwa na askari wa JWTZ walivuliwa nguo zote na kulazwa kifudifudi, kumwagiwa maji ya baridi na kupakwa chumvi kisha kuanza kupigwa usiku kucha kwa kutumia mikanda ya jeshi, ngumi, mateke na fimbo maalum za ngozi za wanyama na miti maalum.

Alisema viongozi hao wakiwa njia kurejea Mtwara Mjini wakitokea Msimbati magari mawili ya jeshi yaliziba barabara baada ya kuliona gari la CUF  na wanajeshi walianza kuwashusha na kuwapiga kisha kuwarusha kwenye karandinga lao.

Alisema baadaye walipelekwa katika kambi ya Naliendele kabla ya kuachiwa saa 5:00 usiku na kukabidhiwa kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.

“Kwa bahati mbaya Mketo alipigwa sana katika ubavu wake wa kulia ambao amewahi kufanyiwa operesheni kubwa miezi kadhaa iliyopita,. 


Alipoona anapigwa sana eneo hilo akaona awaombe askari wampige maeneo mengine lakini eneo hilo wamhurumie, kusikia vile askari wale walimgeuza kwa nguvu na kuanza kumpiga mateke ya nguvu zaidi katika eneo lile hadi alipoteza fahamu,”alisema.
Alisema Mketo alipozinduka Juni 28, mwaka huu  alijikuta ana dripu na hakuelewa ni ya nini na baadaye wanajeshi waliitoa.

Profesa Lipumba alisema tukio la utesaji raia ndani ya kambi ya jeshi ikiliunganishwa na matukio mengine kama ya utesaji wa Dk.Stephen Ulimboka , kutekwa nyara kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), Absalom Kibanda, kulipuliwa bomu katika mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kunadhihirisha hatua za awali za kusambaratika kwa dola.

Msemaji wa JWTZ, Kapambala Mgawe, alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo zinazoelekezwa kwa askari wa jeshi lake,  alisema suala hilo linatiwa chumvi na wanasiasa kwasababu kiutaratibu anayetekwa ni adui hivyo raia wa Tanzania hawezi kutekwa na wanajeshi.

Mgawe alisema tuhuma zinazoelekezwa kwa wanajeshi zina lengo la kutaka kulichafua jeshi hilo ili lisifanye kazi yake kwasababu vipo vipengele vya kisheria vinavyoruhusu askari wa JWTZ kuliingilia kati kudumisha amani kunapotokea Jeshi la Polisi limezidiwa.

Alisema katika kipindi hiki ambacho kuna vurugu nyingi zinajitokeza katika nchini jeshi litakapokuwa linachukua hatua ya kudhibiti yatesemwa mengi ikiwamo askari kuhusishwa na vitendo vya ubakaji.

CHANZO: NIPASHE

Related

TANGAZO MUHIMU KWA WALIMU NA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA SITA MWAKA 2014 KUHUSU KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MWEZI SEPTEMBA 2014

1. Awamu ya pili kwa vijana watakaojiunga na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mujibu wa Sheria itaanza rasmi tarehe 11 septemba, 2014 na itahusisha makundi yafuatayo:- Walimu wote ngazi ya cheti (GA...

CHADEMA: TAMKO KUHUSU KUONDOKA KWA WALIOKUWA VIONGOZI

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Jimbo la Kigoma Kaskazini tunapenda kutoa taarifa kwa umma kutokana na sintofahamu inayotaka kulazimishwa mbele ya jamii kuhusu uimara wa chama che...

CAG AMUITA KAFULILA KUTOA USHAHIDI SAKATA LA IPTL

 Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh MOROGORO.  Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG) amemuandikia barua mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), ...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item