MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA JOHN TENDWA KUKIFUTA CHADEMA

Msajjili wa vyama vya siasa, John Tendwa Hatimaye msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalam...

Msajjili wa vyama vya siasa, John Tendwa
Hatimaye msajili wa vyama vya siasa nchini, John Tendwa ameibuka na kusema sasa anaandaa kalamu yake kukifuta Chama kikuu cha upinzani nchini CHADEMA.
Katika Taarifa yake kwa vyombo vya habari  Tendwa amesema CHADEMA wanataka kuanzisha kikundi cha mgambo ambacho ni kinyume na sheria, katiba ya nchi na sheria za usajili wa vyama.
Msajili huyo amesema kwamba kama madai ya CHADEMA ni kuanzisha kikundi cha kujilinda dhidi ya Green Guard wa CCM madai hayo hayana msingi wowote kwani kama CHADEMA wana taarifa kwamba Green Guard wanahatarisha amani basi wanapaswa kuripoti suala hilo polisi ili lifanyiwe kazi kwa mujibu wa sheria.
Tendwa amezidi kuonya kwamba uamuzi wake ni wa mwisho na atakapoifuta CHADEMA maamuzi yake hayapingwi popote kisheria.

Source:  Global Publishers

Related

OTHER NEWS 3124663515192061162

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item