CCM YAIPONGEZA SERIKALI KWA KUREJESHA BUNGENI MUSWADA SHERIA YA KODI YA TOZO YA LAINI ZA SIMU

A MWANDISHI WETU CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada ...

A MWANDISHI WETU
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeipongeza serikali, kwa uamuzi wake kurejesha bungeni kwa ajili ya mdajala zaidi, muswada wa sheria ulioanzisha kodi mpya ya tozo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu.

Taarifa ya CCM iliyotolewa leo mjini Dodoma, na Katibu wa NEC ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye imesema uamuzi huo umedhihirisha kwamba serikali inawasikiliza na kuwajali wananchi wake.

Akiripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari leo, Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa amekaririwa akisema kwamba mjadala kuhusu muswada wa sheria ya kodi hiyo ya tozo hiyo utafanyika wakati wa mkutano wa Bunge unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Baada ya kupitishwa na bunge Juni mwaka huu, na utekelezwaji wake kuanza rasmi Julai mwaka huu, CCM ilikuwa miongoni mwa wadau waliopinga vikali kuanzishwa kwa kodi ya tozo hiyo, ikieleza kwamba ni mzigo na usumbufu usio wa lazima kwa watumiaji wa simu ambao wengi matumizi yao ni ya kawaida.

Katika taarifa hiyo, CCM imesema kwa kuwa wabunge wengi ni wa chama hicho, watumie fursa hiyo kuhakikisha sheria ya tozo hiyo inaondolewa na wakati huohuo watumie uwezo wao wote kuhakikisha wanaishauri serikali vizuri kupata njia mbadala itakayotumika kuziba nafasi itakayokuwa imeachwa kwa kuondolewa tozo hiyo.

"Kimsingi hatua hii imetupa faraja na hivyo CCM inaipongeza Serikali kwa kuamua kusitisha sheria ya kodi ya tozo hiyo ya sh. 1,000 kwa laini ya simu kwa kuwa ingesababisha usumbufu na adha isiyo ya lazima kwa wananchi", imesema CCM katika sehemu ya taarifa yake.

Source: CCM  Social Media

Related

NEWS ALERT! MSIGWA AACHIWA

Mahakama Iringa imemuachia kwa dhamana Mch. Peter msigwa baada ya kusomewa mashitaka yake hivi punde na kukana shitaka la kujeruhi, kesi imeahirishwa na kutarajiwa kutajwa tena Machi 10, 2013.

MSIGWA AFIKISHWA MAHAKANI LEO

Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mh. Peter Msigwa amefikishwa mahakamani asubuhi hii akihusishwa na vurugu zilizotokea jana jioni akihusishwa na uchochezi wakati wa kampeni za udiwani kata ya Nduli....

IGP MANGU AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI

IGP ERNEST MANGU INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu, amepangua baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa, wapelelezi na wakuu wa polisi wa usalama barabarani, pamoja na watendaji wen...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item