Endapo itatokea Mhe. Edward Lowassa akagombea Urais kweli sintompa kura yangu-Kigwangalla

Mbunge wa jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla- Jana nilialikwa na dada yangu Fina wa Mango kwenye show yake adhimu ya Makutano na...


Mbunge wa jimbo la Nzega,Hamis Kigwangalla- Jana nilialikwa na dada yangu Fina wa Mango kwenye show yake adhimu ya Makutano na Fina Mango. Nianze kwa kumshukuru dada Fina na timu yake kwa kazi nzuri wanayofanya. 

Nimshukuru pia Ndg. Uswege Mwaipyana (my Twitter friend) kwa kupendekeza nialikwe na Fina kwenye show, baada ya yeye (Uswege) kufuatilia ile iliyopita Jumamosi iliyotangulia na kuona ingependeza kama nami ningealikwa. 

Niliongelea mambo mengi ikiwemo historia yangu ya utoto na nilivyougua kwashiakor na marasmus na kuponea chupuchupu kufariki dunia kijijini Goweko, Mlimani kwa babu yangu, elimu yangu na uzoefu wangu kwenye uongozi kwenye taasisi mbalimbali nilizopitia. Niliongelea mapinduzi ya kilimo cha Pamba na Alizeti Nzega ambayo ninayaongoza na pia ndoto zangu za Urais, utendaji wa Rais Kikwete na pia hatma ya Taifa letu kwenye mchakato wa kumpata Rais mpya 2015.

 Dada Fina Mango aliniuliza swali moja lililohusisha Urais 2015 na Mhe. Edward Ngoyai Lowassa (Mb.) ambaye anatajwa tajwa kuwa huenda akawemo among presidential contenders watarajiwa. Majibu yangu yote yalijikita, kama ilivyo kawaida yangu, kwenye ukweli na kwenye tafsiri sahihi ya kimantiki inayotokana na uelewa na utashi wangu. 

Ni kweli nilisema kuwa endapo itatokea Mhe. Edward Lowassa akagombea Urais kweli sintompa kura yangu, sikutafuna maneno, na wala sina chuki ama uadui naye, na nilisema ametenda mengi mazuri na nilisifia ujasiri na umahiri wake kabla ya suala la Richmond, naam kabla ya Richmond saga, niligusia dedication yake, lakini nilihitimisha kwa kusema kuwa kwa zama hizi siwezi kumuunga mkono. Alipofikia panatosha. Naam, panatosha. Kwa kuwa kuna script ya nilichokiongea, acha nikiweke wazi hapa ili wenye kupenda kufuatilia suala hili wajisikilizie wenyewe.

Related

MWANANCHI HUYU WA MWANZA AMKARIBISHA RAIS OBAMA KISTAILI YAKE AKIWA HUKO HUKO MWANZA, HAIJALISHI UMBALI BANA SISI WOTE NI WATANZANIA.

Karibu, karibuKaribu rafiki mkuuKaribu rafiki wa amaniKaribu rafiki mkuu wa IslaelKaribu MuungwanaKaribu Rais Barack ObamaMimi Rafiki wa Israel na USA.PICTURE THANX TO GSENGO

MAANDALIZI YA UJIO WA OBAMA YAKIWA YAMEKAMILIKA, TAYARI KWA MAPOKEZI IKULU JIONEE KATIKA PICHA

KINA MAMA WAMEJAA NA FURAHA KWELIKWELIBARACK OBAMA ROAD KUZINDULIWA RASMI ZULIA JEKUNDU TAYARI KWA UJIOPICHA KWA HISANI YA FATHER KIDEVU

CUF WAJIPANGA KUCHUKUA HATUA DHIDI YA JWTZ, POLICE

CHAMA cha Wananchi (CUF) kimesema kinawasilisha na mawakili wake na asasi za haki za binadamu kujua hatua za kisheria kuchukua dhidi ya  askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mada...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904758
item