JAJI MKUU MSTAAFU KUTOA USHAHIDI DHIDI YA DK. SLAA
Jaji Mkuu Mstaafu kutoa ushahidi jaribio la kumtapeli Willbrod Slaa ******* Hai. Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas Samatta ni miongon...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/08/jaji-mkuu-mstaafu-kutoa-ushahidi-dhidi.html
Jaji Mkuu Mstaafu kutoa ushahidi jaribio la kumtapeli Willbrod Slaa
*******
Hai. Jaji Mkuu Mstaafu,Barnabas
Samatta ni miongoni mwa mashahidi 12 watakaotoa ushahidi katika kesi ya
jinai ya jaribio la kumtapeli Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willbrod Slaa.
Wengine watakaotoa ushahidi katika
kesi hiyo inayomkabili Abedi Adam Abedi (22) ni Dk Slaa mwenyewe na
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema.
P.T
Orodha ya majina ya mashahidi hao
ilitolewa mahakamani juzi mbele ya Hakimu Mkazi wa Wilaya ya Hai, Denis
Mpelembwa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Maghela Ndimbo.
Wengine watakaotoa ushahidi ni wakili
mashuhuri wa Chadema, Profesa Abdalah Safari, Rumisha Slaa, Happynes
Masue, Godfrid Njau, Gervas Geneya, Neema Godbless,Aron Misanga, Prosper
Mbilinyi na Judith Mashashi.
Akisoma maelezo ya awali, Ndimbo
alidai kuwa kati ya Aprili na Mei, 2012, mshtakiwa alijitambulisha kwa
Dk Slaa, Lema na Profesa Safari kuwa yeye ni mtumishi wa Takukuru.
Ilidaiwa kuwa katika kipindi hicho,
mshtakiwa aliwapigia simu Dk Slaa, Lema na Profesa Safari na
kujitambulisha kuwa yeye ni Abel Kibaso Mkuu wa Takukuru Wilaya ya
Ulanga.
Katika kipindi hicho pia, mshtakiwa
aliwapigia simu viongozi hao akijitambulisha ni Jaji mstaafu Samatta
akitaka wampe pesa ili washinde katika kesi iliyokuwa mahakama ya Rufaa.
Rufaa hiyo namba 47/2012 ilifunguliwa
na Lema dhidi ya Mussa Hamisi na wenzake akipinga hukumu ya Mahakama Kuu
Arusha ya kupinga kuvuliwa Ubunge wa Arusha mjini kesi ambayo kwa sasa
ilishatolewa uamuzi.
mashtaka huyo alidai mahakamani kuwa
mshtakiwa alijifanya ni Jaji Mkuu Mstaafu Samatta wakati akijua siyo
Jaji Samatta kwa lengo tu la kujipatia fedha kinyume cha sheria.
Hata hivyo Lema alishinda Rufaa hiyo na kurudishiwa Ubunge wake.
Mshtakiwa amekanusha mashtaka hayo na
kesi hiyo imepangwa kuanza kusikilizwa rasmi Septemba 25 ambapo Jaji
Samatta ni miongoni mwa mashahidi wa upande wa Jamhuri.