TCRA YAZIFUNGULIA REDIO IMAAN YA MOROGORO NA KWA NEEMA YA MWANZA
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) leo imezifumgulia Redio Imaan ya Morogoro na Kwa Neema inayorusha matangazo yake kutoka jijini Mwanza, zil...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/08/tcra-yazifungulia-redio-imaan-ya.html
Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) leo imezifumgulia Redio Imaan ya Morogoro na Kwa Neema inayorusha matangazo yake kutoka jijini Mwanza, zilizokuwa zimefungiwa kwa muda wa miezi 6 kutokana na sababu za kuhatarisha amani. Pata taarifa rasmi hapa chini.
JAMHURI
YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUREJESHWA
KWA URUSHAJI MATANGAZO RADIO IMAAN FM NA KWA NEEMA FM RADIO
1.0
Utangulizi:
Mnamo
tarehe 26/02/2013 Kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilitoa
uamuzi wa kuvifungia vituo vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na
Kwa Neema FM Radio ya jijini Mwanza baada ya kukiuka Sheria na Kanuni za
Utangazaji.
Kamati
ya Maudhui iliuita uongozi wa vituo hivyo tarehe 11/02/2013 na tarehe
14/02/2013 ili kujitetea na vyote vilikiri kosa. Baada ya kutafakari utetezi wa
Radio Imaan na Radio ya Kwa Neema FM na kwa kuzingatia Sheria na Kanuni za
Utangazaji, Kamati iliamua kutoa adhabu kwa vituo vyote viliwi kama ifuatavyo:-
a)
Vituo vyote vilipewa onyo pamoja na kufungiwa kurusha matangazo kwa kipindi cha
miezi sita kuanzia tarehe 26/02/2013;
b)
Vituo vyote vilitakiwa kuithibitishia Mamlaka ya Mawasiliano na Kamati ya
Maudhui kwa maandishi kuwa hawatarejea kutenda kosa la aina hiyo au
linalofanana na hilo. Ikiwa vitarudia Kamati ya Maudhui haitasita kuvifutia
leseni zao za utangazaji.
2.0
Kutekeleza adhabu na hatua zilizochukuliwa na vituo hivyo
na
Mamlaka ya Mawasiliano:
Baada
ya Uamuzi huo kusomwa, vituo vyote viwili vilianza kutekeleza adhabu mara moja
kama ilivyotakiwa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za Utangazaji. Mamlaka ya
Mawasiliano ilipokea barua ya udhibitisho wa kutofanya kosa tena yaani
“Commitment letter” pamoja na sera ya uhariri (Editorial Policy) na ratiba ya
vipindi kutoka kwa vituo vyote viwili.
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania ilifanya ukaguzi kwa vituo vyote viwili ili kujiridhisha
na kuzipitia sera za uhariri pamoja na mwongozo wa vipindi kabla ya
kuvifungulia.
3.0
Kurejeshwa kwa Matangazo
Kamati
ya Maudhui iliandika barua tarehe 27/08/2013 kuhusu kuvifungulia vituo hivyo
vya utangazaji vya Radio Imaan ya mjini Morogoro na Kwa Neema FM Radio ya
jijini Mwanza baada ya kutumikia adhabu kwa mujibu wa Sheria na Kanuni za
Utangazaji. Vituo hivi vimeanza kurusha matangazo yake kuanzia leo tarehe
28/08/2013 baada ya muda wa adhabu kuisha.
Kamati
ya Maudhui inapenda kutumia fursa hii kuvionya vyombo vya habari vya utangazaji
vya redio na televisheni kuwa makini katika kutekeleza masharti ya leseni
pamoja na kufuata Sheria na Kanuni za Utangazaji. Kamati ya Maudhui haitasita
kutoa adhabu kali au kuvifungia vituo vitakavyokiuka Masharti ya leseni, Sheria
pamoja na Kanuni za Utangazaji au hata kuvifutia leseni zao.
Kamati
ya Maudhui inatoa wito kwa vyombo vya habari vya utangazaji kuzingatia Sheria,
Kanuni na Masharti ya leseni ilikuboresha Sekta ya Utangazaji na kudumisha
amani nchini.
Eng.
Margaret Munyagi
Mwenyekiti,
Kamati
ya Maudhui Ya TCRA,
S.L.P.
474,
DAR
ES SALAAM.
28/08/2013
KUHUSU
KAMATI YA MAUDHUI:
1.0
UTANGULIZI:
1.1.
Kamati ya Maudhui ni kamati iliyoundwa kwa mujibu wa sehemu ya IV kifungu cha
26 (1) cha Sheria Namba 12 ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ya mwaka 2003, na
marekebisho yake katika kifungu 173 cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki
na Posta (EPOCA) Mwaka 2010
Kwa
mujibu wa sheria, majukumu na kazi za Kamati ya Maudhui ni pamoja na:-
(a)
Kumshauri Waziri wa Sekta kuhusiana na Sera ya Utangazaji nchini;
(b)
Kushughulikia malalamiko kutoka kwa watangazaji na watumiaji wa huduma za
utangazaji nchini;
(c)
Kusimamia na kuhakikisha kuwa kanuni za utangazaji zinafuatwa.
(d)
Kusimamia na kufuatilia maudhui ya vituo vya utangazaji.
1.2.
Kamati hii ilianza kazi zake Oktoba 2012 baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Fenella Mukangara (MB) tarehe 4
Desemba, 2012.
1.3.
Kamati ya Maudhui inaundwa na wajumbe watano. Wanne ni wateuliwa wa Waziri
mwenye dhamana ya Sekta ya Utangazaji na Mwenyekiti ambaye huchaguliwa miongoni
mwa wajumbe wa Bodi ya TCRA. Muundo huo umetolewa na sehemu ya 26 (2) ya Sheria
ya TCRA ya Mwaka 2003.
Majina
ya wajumbe ni kama ifuatavyo:-
i.
Mhandisi Margareth Munyagi -Mwenyekiti
ii.
Bwana Walter Bgoya -Makamu Mwenyekiti
iii.
Bwana Abdul Ngarawa -Mjumbe
iv.
Bwana Joseph Mapunda -Mjumbe
v.
Bwana Yusuf Nzowa -Mjumbe