TASWIRA ZA MATUKIO MBALIMBALI KATIKA ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM HUKO TARIME MKOANI MARA
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoan...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/09/taswira-za-matukio-mbalimbali-katika.html
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara. |
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana ,jana alifanya ziara katika wilaya ya Tarime Mkoani Mara . Katibu Mkuu akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.
Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.
- Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo
- Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.
- Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi. Fatilia ziara hiyo katika picha chini.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma moja ya taarifa inayofafanua matatizo ya wakazi wa Nyamongo. |
fisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi jana tarehe 23 Septemba 2013.. |