ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM ABDULRAHMAN KINANA NA KATIBU MWENEZI NAPE NNAUYE MKOANI SHINYANGA KATIKA PICHA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja akimlipa ujira wa shilingi elfu 10.000 Katibu wa NEC Itikadi S...


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja akimlipa ujira wa shilingi elfu 10.000 Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye baada ya kumsaidia katika ujenzi wa Birika la kunweshea mifugo katika kata ya Didia, hata hivyo Kinana aliwapa fedha pia wajenzi wa birika hilo.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasalimu wananchi waliofika kumpokea kwenye wilaya ya Kishapu katika eneo la Maganzo ambapo Katibu Mkuu alikuwa na ziara katika wilaya ya Kishapu.

Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kupaka rangi moja ya madarasa katika shule ya Sekondari Mwigumbi.

Moja ya Nyumba mpya iliyojengwa kwa ajili ya makazi ya Walimu wa Shule ya Sekondari Mwigumbi, wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga ambayo ilizinduliwa  na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Mbunge wa jimbo la Solwa Ahmed Salum wakicheza na nyoka pamoja na wanakukundi cha utamaduni kutoka jimboni humo

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye wakishiriki katika ujenzi wa Birika la Kunyweshea mifugo linalojengwa katika Kata ya Didia Jimbo la Solwa Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga vijijini  Shinyanga 1


Burudani

Kinana akizungumza na wananchi waliomsimamisha katika kijiji cha Mwabenda ambao walikuwa na mabango yaliyokuwa yakielezea kero zao katika kijiji hicho ambazo zilikuwa ni Umeme na maji hata hivyo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ndugu Ally Rufunga aliwaelezea mipango ya serikali kuhusu kijiji hicho katika kuhakikisha maji na umeme vinapatikana mapema katika kijiji hicho

Sanaa ilichukua nafasi yake




Katibu wa NEC Itikadi Siasa na Uenezi CCM Ndugu Nape Nnauye akiwahutubia wananchi waliojitokeza katika mkutano huo

Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika kijiji cha Salawe kwenye mkutano wa hadhara.

Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wakati alipokagua ujenzi wa Soko la Kata ya Didia lililojengwa katika kijiji cha Didia, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Ndugu Khamis Mngeja.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mbele ya soko hilo.




Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahma Kinana akichekecha mchanga wa kujengea darasa katika shule ya sekondari ya Mwigumbi,Katibu Mkuu amekuwa akishiriki katika shughuli za kijamii hasa zinazohusu utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa CCM.

Related

NEC KUTANGAZA TAREHE YA UCHAGUZI JIMBO LA KALENGA

JULIUS MALABA - MKURUGENZI WA UCHAGUZI Dar es Salaam. Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema wiki hii itatangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kalenga, lililopo wazi baada ya ...

USIKU WA WASANII NA WANAHABARI WAFANA, TAZAMA PICHA ZA TUKIO HILO

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na wageni waalikwa kwenye sherehe za Usiku wa Wasanii na Waandishi wa Habari zilizofanyika usiku wa tarehe 2 Februari kwenye ukumbi ...

RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE APOKEA HUNDI YA SHILINGI MILIONI 100 ILIYOTOLEWA NA BENKI YA CRDB KUSAIDIA WALIOATHIRIKA NA MAFURIKO MKOANI MOROGORO

   Rais Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete akipokea Hundi ya Shilingi Milioni 100 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, kusaidia waathirika  wa mafuriko...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904788
item