JAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI NCHINI AAPISHWA KUWA JAJI WA MAHAKAMA YA KIMATAIFA YA MAKOSA YA JINAI (ICC)YA NCHINI CAMBODIA

AJI wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.Dr. Stephen Bwana ameapishwa leo (Alhamisi) kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC...

AJI wa Mahakama ya Rufani (T), Mhe.Dr. Stephen Bwana ameapishwa leo (Alhamisi) kuwa Jaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) ya nchini Cambodia. 

Uapisho huo unafuatia baada ya kuteuliwa kwake na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, 
Mhe. Ban. Ki Moon kwa kushauriana na Mfalme wa Cambodia, Mtukufu Norodom Sihamoni
mnamo tarehe. 09.05.2012.

Kabla ya uteuzi huo Dr. Bwana ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani (T) aliwahi kushika nafasi mbalimbali Kama Jaji wa Mahakama Kuu, Seychelles, 1994-1999, Jaji
wa Mahakama ya Rufaa ya Seychelles 2004-2009, pia Kaimu Rais wa Mahakama hiyo ya Rufani
kuanzia Mwaka 2006-2008.

Mbali na kushika nyadhifa hizo, Dr. Bwana pia aliwahi kuwa, Mshauri wa Benki ya Dunia Kuhusu
uboreshaji wa shughuli za Mahakama, Afrika (2003-2008), Msajili, Mahakama ya Rufani (T),
1989-1994, Msajili, Mahakama Kuu ya Tanzania 1989 na Hakimu Mkazi 1974.

Related

OTHER NEWS 2729404443445440162

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item