WAHITIMU WA VYUO VYA ELIMU YA JUU WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI MWAKA 2013/2014 BAADA YA USAILI KUKAMILIKA
1.Wahitimu wataondoka tarehe 19/11/2013 kwenda Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi, mabasi yataondoka Polisi Ufundi Dsm saa 06.00 asubuh...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/11/wahitimu-wa-vyuo-vya-elimu-ya-juu.html
1.Wahitimu
wataondoka tarehe 19/11/2013 kwenda Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi,
mabasi yataondoka Polisi Ufundi Dsm saa 06.00 asubuhi. Mwisho wa
kuriporti Chuoni ni tarehe 23/11/2013. Atakayeripoti kuanzia tarehe
24.11.2013 atahesabika amechelewa hatapokelewa chuoni hapo.
2.Vijana hawa watalazimika kufika chuoni wakiwa na mahitaji yafuatayo:
a)
Vyeti vyao vyote vya masomo( original Academic Certificates/Result slip
pamoja na Leaving certificates) kidato cha Nne/Sita, Vyeti vya kuzaliwa
(Original Birth certificates). Hati ya kiapo cha kuzaliwa
haitakubalika.
b) Mashuka mawili rangi ya Bluu Bahari (light blue)
c) Chandarua chenye upana futi tatu
d) Nguo za michezo(Track suit nyeusi,Tshirt blue na Raba)
e) Pasi ya Mkaa
f) Ndoo moja
g) Pesa za kulipia bima ya afya kiasi cha shilingi elfu hamsini na mia nne tu (50,400/=). Aliyemwachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya hatalazimika kulipia kiasi hiki cha fedha.
h) Pesa kidogo ya kujikimu.
3.
Kwa mujibu wa kanuni za chuo ni marufuku kufika chuoni na simu ya
mkononi au kifaa chochote cha mawasiliano. Atakayepatikana na simu
atafukuzwa chuoni hapo. Chuo kitaelekeza na kusaidia kufanya
mawasiliano.
4.Kuona orodha bofya hapa ;