DKT. ASHA - ROSE MIGIRO AAPISHWA BUNGENI LEO

MBUNGE wa kuteuliwa na Rais,  Dk. Asha-Rose Migiro, leo saa 3 asubuhi, ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania. Akizungumza nje ya ...

MBUNGE wa kuteuliwa na Rais,  Dk. Asha-Rose Migiro, leo saa 3 asubuhi, ameapishwa kuwa mbunge wa Bunge la Tanzania.

Akizungumza nje ya viwanja vya Bunge, baada ya kuaspishwa, na Spika wa Bunge Anna Makinda,  Dk. Asha-Rose ameahidi utumishi wenye uadilifu, uaminifu na wa kujituma.

Alisema  ubunge ni uwakilishi uwe wa kuteuliwa, kupitia viti maalum au majimbo na kwamba nafasi hiyo aliyopewa sio ya kwake binafsi bali ni heshima kwa wanawake wote nchini.

"Unapopewa fursa kama hiyo sio yako binafsi bali ni heshima ya wanawake wote kwa sababu nimeongeza idadi ya waliopo bungeni’’

“Hivyo ni nafasi nyingine kuwa wanawake tunawajibu na tunapopata fursa basi tuna kila sababu ya kutumikia umma na Nchi yetu kwa moyo wote na kwa nguvu zote,"alisema Dk. Migiro.

Kwa  mara nyingine Dk. Migiro alimshukuru  Rais Dk. Jakaya  Kikwete  kwa uteuzi wake kwake kwa kuwa umempa  heshima na fursa nyingine ya kutumikia  Taifa.

"katika maisha mtu anaweza akafanya kazi yoyote na kazi yoyote ina thamani lakini nafikiria kazi ya kutumikia umma ni heshima ya pekee kwa sababu kama utaweza kufanya shughuli kwa ufanisi basi matokeo yake yanasambaa kwa watu wengi zaidi,"aliongeza Dk. Migiro.

Related

CHADEMA WATOA SIKU TATU KWA RAIS KIKWETE

  Benson Kigaila akiongea na wanahabari Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kufuta kauli yake ya kuwataka wana CCM kuacha unyonge na kujibu mapigo dhidi ya upinzani na ametakiwa kuomba radhi nd...

BUNGE LA KATIBA VIPANDE VIPANDE

Wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wakijiandikisha bungeni mjini Dodoma, ikiwa ni maandalizi ya kuanza kwa vikao vya bunge hilo. Picha na Silvan Kiwale  Dodoma. Bunge Maal...

POLISI WAPONGEZWA KUPUNGUZA UHALIFU

 Na Kija Elias, Moshi. SERIKALI imelipongeza jeshi la polisi kwa kupunguza uhalifu wa kimataifa kufikia asilimia 1.1 tofauti na ilivyokuwa mwaka 2012. Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nc...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item