KRISMASI 2013: PAPA FRANCIS ATETEA WANYONGE WA VITA
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani. Alitoa wito kwa pande z...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/krismasi-2013-papa-francis-atetea.html
Katika hotuba yake ya mwanzo ya Krismasi, Papa Francis amezungumza mjini Rome juu ya maeneo ya vita duniani.
Alitoa wito kwa pande zote zilizohusika na vita vya Syria ziruhusu msaada kufika kwa wanyonge.
Alisema:
"Maisha mengi yamevunjika katika vita vya Syria na kuchochea chuki na kulipiza kisasi.
Wacha tuendelee kumuomba Mungu awaepushe
wapendwa watu wa Syria na maafa zaidi, na kuziwezesha pande zilizohusika
na vita kumaliza ghasia na kuruhusu msaada ufike kwa wale wanaouhitaji"
Papa Francis piya alitoa wito kwa mapigano
kusitishwa Sudan Kusini na aliwaomba viongozi wa kimataifa kushughulikia
zaidi yanayotokea Jamhuri ya Afrika ya Kati ambayo alisema mara nyingi
haitiwi maanani.
Akizungumza juu ya mamia ya wakimbizi kutoka
Eritrea waliozama karibu na kisiwa cha Utaliana cha Lampedusa mwezi
Oktoba, alieleza wasiwasi wake kuhusu wale wanaohatarisha kila kitu ili
kutafuta maisha bora. Piya alizungumzia swala la ukatili majumbani, akitetea wanawake wanaopigwa.