MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI, ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA MZEE MANDELA
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akitia saini kitabu cha maombolezo ya Kifo cha Mpigania Uhuru wa Afrika kusini Rais wa K...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2013/12/makamu-wa-pili-wa-rais-wa-zanzibar.html
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiagana na Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdullrahman Kinana tayari kupanda ndege kuelekea Nchini Afrika Kusini.akifuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi |
Na Othman Khamis Ame OMPR
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi
Seif Ali Iddi ameondoka Nchini leo jioni kuelekea Johannesburg Afrika
ya Kusini kwa ajili ya kuhudhuria sala Maalum ya pamoja ya kuuaga mwili
wa Kiongozi mashuhuri Duniani Rais Mstaafu wa nchi hiyo Mzee Nelson
Mandela.
Sala hiyo maalum
inayotarajiwa kufanyika kesho kwenye uwanja maarufu wa NFP nchini Afrika
Kusini inatarajiwa kuhudhuria na Viongozi kutoka zaidi ya nchi sabini
Ulimwenguni.
Kwenye uwanja wa ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Jijini Dar es salaam Balozi Seif
aliagwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndg. Abdullrahman Kinana
pamoja na baadhi ya Viongozi wa Kisiasa na Serikali zote mbili za SMT na
SMZ.
Balozi Seif
aliyefuatana na Mkewe Mama Asha Suleiman Iddi akimuwakilisha Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein ni
miongoni mwa Ujumbe wa Tanzania utaoshiriki tukio hilo ukiongozwa na
Rais wa Jamuhuri yaMuungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar anatarajiwa kurejea Zanzibar kesho kutwa jioni ya Tarehe 11 mwezi Novemba mwaka 2013.
Marehemu Mzee Nelson
Madela anayetarajiwa kuzikwa Jumapili ijayo alikuwa Kiongozi shupavu wa
Afrika Kusini aliyesimama imara kuongoza mapambano dhidi ya ubaguzi wa
rangi uliokuwa ukiendeshwa na Makaburu waliyokuwa wakiitawala nchi hiyo.
Harakati hizo za Mzee
Mandela zilipata nguvu kutokana na msaada wa baadhi ya viongozi kadhaa
Barani Afrika ambazo hatimaye Makaburu hao wakaamua kumfungulia
mashtaka na kufungwa jela kwa takriban miaka 27 katika Kisiwa cha Robin
ambacho sasa kimekuwa sehemu kubwa ya Utalii Nchini Afrika Kusini.
Kiongozi huyu ambae ni
wa aina yake hapa Duniani alisimama imara kudai haki za watu weusi
waliokuwa wakinyanyaswa na kukandamizwa kwa sababu tu ya rangi yao.
Credits: ZanziNews