TASWIRA MBALIMBALI MAADHIMISHO MIAKA 52 YA UHURU WA TANGANYIKA, RAIS KIKWETE ATOA MSAMAHA KWA WAFUNGWA 1400

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua a...

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania  uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama.

Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru

Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.

Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.


Wananchi walijitokeza kwa wingi kushuhudia

Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”.

Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.

Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.

Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.

Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) .


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO)

Katika kuadhimisha miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika, Rais Kikwete ametoa msamaha kwa wafungwa wapatao 1400 katika magereza mbalimbali nchini.

PICHA NA ARON MSIGWA - MAELEZO.

Related

DKT. SHEIN AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA INDIA MOHAMMED HAMID ANSARI

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed  Shein akifuatana na Balozi wa Tanzania Nchini India John W.H.Kijazi walipofika katika Makumbusho ya Mahatma Ghan...

ALICHOANDIKA JOYCE KIRIA KWA FACEBOOK PAGE YAKE BAADA YA BAADHI YA WASANII WA BONGO MOVIE KUJIUNGA NA CCM

 Hawa ni baadhi ya  wasanii walioshiriki sherehe za miaka 37 CCM mkoani mbeya jana, na kuamua kujiunga na chama tawala cha CCM. Bi Joyce Kiria akaamua kuandika maoni yake kuhusu tukio hil...

MBEYA CITY YAAMBULIA PATUPU KWA YANGA, YAFUNGWA 1 - 0

TIMU ya Mbeya City leo imepokea kipigo cha kwanza katika Ligi Kuu ya Bara baada ya kulala kwa bao 1-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Bao pekee la Y...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904763
item