KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM ZANZIBAR LEO

  Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilich...

 Mwenyekiti wa CCM Taifa Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua kikao cha siku moja cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kilichofanyika leo mjini Zanzibar ,pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na wananchi wake kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari wa mjini Zanzibar kuhusu yale yaliojiri kwenye kikao cha Kamati Kuu ya Halmashuri Kuu ya CCM Taifa na pia kutangaza uteuzi wa Ndugu Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa imekuwa na kikao cha siku moja leo tarehe 13/01/2014 mjini Zanzibar chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Dr. Jakaya Kikwete.
Pamoja na mambo mengine Kamati Kuu imeipongeza sana Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, wazanzibari na watanzania kwa ujumla kwa kuadhimisha miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Aidha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imepongezwa kwa maandalizi mazuri na ya kufana ya sherehe hizo.
 
Kamati Kuu imetambua na kupongeza hatua kubwa ya maendeleo iliyofikiwa tangu mapinduzi mwaka 1964 mpaka leo. Wito umetolewa kuyalinda na kuyaendeleza mema yote yatokanayo na mapinduzi hayo na mafanikio yaliyoletwa na serikali inayoongozwa na CCM.

Aidha Kamati Kuu imemteua Ndg. Mahmoud Thabit Kombo kuwa mgombea wa uwakilishi jimbo la Kiembesamaki kupitia CCM.

Kesho mgombea huyu wa CCM atachukua fomu za tume za kugombea. Uzinduzi wa kampeni za CCM utafanyika tarehe 22/01/2014 kwenye viwanja vya Kiembesamaki ambapo mgeni rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndg. Mohamed Gharib Bilal.
 
Kampeni za CCM zitafungwa tarehe 01/02/2014 huko Chukwani na mgeni Rasmi atakuwa Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Ndg. Balozi Seif Ali Idi.
 
Kampeni itaendeshwa na Kamati ya Siasa ya wilaya ya Dimani viongozi na wanachama wa wilaya husika, na ngazi zingine za Chama zitashirikiana na ngazi ya wilaya kuhakikisha CCM inashinda tena jimbo hili.
Kamati Kuu inawatakia kila la kheri kwenye kampeni na hatimaye uchaguzi huo. Kampeni na hata upigaji kura uendeshwe kwa amani na utulivu kama ulivyo utamaduni wetu.
   
Imetolewa na;
Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi
13/01/2014

Related

OTHER NEWS 7566769236372397473

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item