KUTEKWA NA KUTESWA MWENYEKITI WA TEMEKE, MPANGO MZIMA WA KUIHUSISHA CHADEMA HUU HAPA
J ana majira ya saa 3.30 asubuhi, watu wapatao watano ambao ni wanachama wa CHADEMA mamluki wa Timu ya Zitto na CCM, wakiwa eneo moja ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/kutekwa-na-kuteswa-mwenyekiti-wa-temeke.html
Jana
majira ya saa 3.30 asubuhi, watu wapatao watano ambao ni wanachama wa
CHADEMA mamluki wa Timu ya Zitto na CCM, wakiwa eneo moja la ofisi ya
umma wakisubiri huduma ya muhimu sana, walipokea simu ya taarifa kuwa
Mwenyekiti wao wa chama wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick alikuwa
amekutwa mahali fulani Dar es Salaam baada ya kutekwa, kuteswa na
kuumizwa na watu wasiojulikana.
Wale
watu mara tu baada ya kupokea habari hizo, wakamtafuta mtu waliyekuwa
wakimwita kwenye simu jina la Mchange (wala si mwingine ni Mhange huyo
huyo anayefahamika katika masuala hayaya circles za usaliti dhidi ya
CHADEMA).
Wakamwambia
habari hiyo (inavyoonekana yeye alikuwa tayari anaijua na alikuwa
mahali fulani kwa mwanasheria). Akawauliza wanaweza kumtaja mtu (a watu)
yeyote wanayetaka ahusishwe kwenye tukio hilo kisha afunguliwe kesi.
Mtu ambaye akihusishwa itakuwa rahisi kwa viongozi wakuu wa chama na
hatimaye chama kizima kuhusishwa kwenye tukio hilo.
Wale
watu wakamwambia ili kumalizana na ‘biashara’ ya CHADEMA kabisa kwa
kuwahusisha viongozi na hatimaye chama kizima katika tukio hilo ambalo
linaweza kukuzwa na kuoneshwa kuwa ni UGAIDI, wako tayari kumtajia
majina ya watu wawili ambao wamekuwa wakikihami na kukitetea sana
CHADEMA Temeke, hivyo ni kikwazo kwa mikakati yao ya kukihujumu CHADEMA
katika eneo hilo.
Kama inavyojulikana kwa upande wa Dar es Salaam, mikakati ya kuihujumu CHADEMA imekuwa ikifanyika kwa kiasi kikubwa sana Temeke.
Wale
watu wakamtajia huyo mtu waliyekuwa wakimtaja kwa jina la Mchange,
majina ya watu wawili, Mzee Salum Zinga na Bernard Mwakyembe. Wote hawa
ni makamanda kweli kweli hapo Temeke, kiasi kwamba Mwenyekiti wa sasa wa
CHADEMA Wilaya ya Temeke amekuwa akimhofia sana Mwakyembe kwamba
anaweza kuchukua nafasi yake wakati wa uchaguzi ujao wa ndani ya chama
hicho.
Baada
ya kumtajia majina hayo, wakamwambia wanapitia ofisi ya wilaya ya chama
hicho mara moja, kisha wakutane kituo cha polisi ili wakafungue
malalamiko dhidi ya watu hao wawili kuwa wamehusika na tukio la kutekwa,
kuteswa na kuumizwa kwa mwenyekiti huyo. Mpango mzima ukawa umekamilika
na ukatekelezwa.
Tunavyozungumza
hapa sasa tayari Mzee Salum Zinga ambaye ni Mwenyekiti wa Wazee Jimbo
la Temeke ameshakamatwa na polisi na sasa jeshi hilo linamtafuta
Mwakyembe. Lakini kwa namna ambavyo mpango huo umepangwa na
utakavyotekelezwa, lengo ni kuwafikia viongozi wa juu.
Mpango
huo uliozungumzwa na watu hao watano pale Temeke kwa kuwasiliana na
Mchange ndiyo msingi wa kauli za Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar
es Salaam, Suleman Kova, kutamka kwa kuihusisha CHADEMA huku akijigamba
kuwa watamkamata mtu yeyote bila kujali cheo chake. Akilenga viongozi
wakubwa wa chama hicho.
Huyo
Kova ambaye kwa sababu ameshajitambulisha kuwa ni bingwa wa kugeuza
matukio haya ya ukatili kuwa ni ‘filamu’ ya kuficha ukweli na kuanza
kusaka uongo, hatuna haja ya kumjadili zaidi ya hapo. Ila ajue tu kuwa
mpango mzima unajulikana.
Ndiyo
maana sehemu ya mpango huo ni kumlazimisha Yona arudi na kulazwa Moi
ambako alikuwa ameagwa jana hiyo hiyo baada ya kubainika hana majeraha
makubwa na angetakiwa kurudi baada ya wiki mbili. Hiyo ilikuwa ni baada
ya CHADEMA kuwa wamesimamia matibabu yake, ikiwemo kumlipia gharama za
hospitali na usafiri kumpeleka nyumbani.
Akiwa
hapo hospitalini amezungumza na vyombo vya habari kwa namna tofauti
tofauti, kwa mtazamo wa kila chombo na kadri ya maelekezo…
Mpango mzima unaandaliwa pia kupitia vyombo vya habari;
Angalia kutoka magazetini
Kama
mlivyoona leo kwenye kurasa za mbele za magazeti yote yaliyotoka leo,
habari hii imepewa uzito mkubwa, ingawa kwa namna tofauti tofauti,
kulingana na uwezo, sera za vyombo vya habari na MALENGO ya chombo husika, hasa katika kufanya kazi za watawala dhidi ya CHADEMA.
Lengo
lingine ni kubeba agenda za makundi ya kuwania urais ndani ya CCM,
ambayo CHADEMA ndiyo tishio pekee la wao kufanikiwa kwenda ikulu, hivyo
yanafanya kila jitihada kukiumiza chama hicho kwa propaganda nyepesi
kama ya tukio hilo.
Kwa
upande wako fanyia kazi PICHA zilizotumika leo katika magazeti yote.
Zimepigwa wakati gani? Eneo gani? Saa ngapi huyo mpiga picha maalum
alikuwa ameandaliwa kwa ajili ya kupiga hizo picha zinazooenakaana
kupigwa kwa ustadi na kifaa kizuri? Kuna maswali mengi sana ukizingatia
kuwa picha zilizotumika katika habari hiyo ni za aina moja! Nani
kazipiga?
Hapa tunaweza kujadili habari kutoka katika magazeti kadhaa;
Endelea......
Mtanzania
Gazeti hili limeipatia habari hii kichwa kisemacho INATISHA. Ndani
ya habari gazeti hilo kwa malengo linalojua yenyewe, labda likiongozwa
na kile kinachoweza kuitwa aina ya weledi wa aina yake wa taaluma ya
habari, sera za chombo hicho na malengo ya wamiliki, limewahusisha
viongozi wa CHADEMA katika tukio hilo kwa hali ambayo inaacha maswali
mengi sana.
Mathalani kwenye moja ya nukuu zake, wamemnukuu Yona akisema
“Bernard
na Mwakyembe walinisalimia na kuondoka, baada ya hapo, wakaja watu
wengine wane ambao siwajui, wakajitambulisha kwangu kuwa ni polisi
wanatoka kituo cha kati, hivyo basi wananihitaji kwa ajili ya
mahojiano.”
Waandishi
wa gazeti hili wangekuwa na nia ya kufanya uandishi unaowajibika kwa
jamii, wangefanya kazi yao kidogo tu wangebaini kuwa Yona katika hilo
alikuwa amewadanganya au amewaambia kitu ambacho kinahitaji kufanyiwa
kazi zaidi.
Kwa
sababu kama umefuatilia mtiririko wa taarifa hii, kuna mtu anaitwa
Bernard Mwakyembe (mtu mmoja), lakini hapa Yona ametaja kwamba hao ni
watu wawili tofauti. Gazeti lilipaswa kufanya kazi yake badala ya
kutumika kuwa karatasi ya kufanyia propaganda za CCM dhidi ya CHADEMA.
Katika
aya mbili zinazofuata ndiyo zinaliacha gazeti hilo uchi kabisa kwamba
limeamua kutumika kwenye mkakati unaoandaliwa na CCM kupitia vyombo vya
dola. Limeandika hivi;
“Tulibishana
sana tena ni muda mrefu, mwisho nikawaambia wanionyeshe kibali cha
kunikamata lakini walinijibu kuwa wao ni polisi, napaswa kutii amri kama
kuna mahojiano zaidi yatafanyika kituoni, nikapanda gari lao na
kuondoka,” alisema Patrick.
Soma
na aya inayofuata ambayo gazeti hilo limeandika kama vile lilikuwepo
wakati tukio linatokea. Kwa sababu lilipaswa kuandika maneno ya Yona ni
madai…allegations.
“Alipohoji
sababu ya watu hao kujitambulisha ni polisi wakati anawajua kuwa si
wanausalama, walianza kumshurutisha kuingia ndani ya gari alipogoma
walimsukuma kwa nguvu ndani ya gari hilo na kumwambia kuwa wanampeleka
kituo cha kati.”
Aya
hizo mbili zilitosha kabisa kuwashtua waandishi au wahariri makini kuwa
chanzo cha habari wanachozungumza nacho si cha kuaminika au kinazua
maswali mengi mno.
Mtu
aliyesema dakika kadhaa tu zilizopita kuwa walikuja watu wengine wanne
hawajui, wanajitambulisha kuwa ni polisi, akawahoji vitambulisho,
wakashindwa kutoa, akabishana nao sana maeneo ya baa (hakuna mtu
aliyesikia?), cha ajabu akakubali kuondoka nao wakati yeye hawajui ni
akina nani, ghafla tena anasema kuwa anawajua kuwa si wanausalama. Kuna
maswali mengi sana?!
Kwa
ujumla habari nzima ya Mtanzania kuhusu tukio hili, ilistahili
kuandikwa na yale magazeti ‘crap’ ya ajabu ajabu yaliyoko mtaani, chini
ya waandishi na wahariri ambao hawajui wala hawathamini chembe hata moja
ya maadili achilia mbali weledi wa kitaaluma.
Wameandika
habari ile badala ya kutumia madai ya nafsi ya tatu umoja, wao
wameandika kama vile walikuwepo hatua kwa hatua na mlalamikaji Yona,
lengo zima ikiwa ni kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na chama hicho
katika sakata zima. Je Mtanzania maslahi yao katika hili ni yapi? Bila
shaka ni makubwa sana.
Angalia aya hizi zilivyoandikwa kwa makusudi, kimkakati;
Patrick
ambaye ni rafiki wa karibu na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA,
Zitto alisema kuwa mgogoro wake na viongozi wakuu wa chama hicho ulianza
tangu alipoitisha mkutano na waandishi wa habari wa kuitaka Kamati Kuu
ya chama hicho kuitisha mkutano wa kujadili suala la kina Zitto, Samson
Mwigamba na Dk. Kitila Mkumbo.
“Niliitisha
mkutano ule ili kuwaambia viongozi wa CHADEMA kujadili suala la kina
Zitto, Kitila na Mwigamba ndani ya chama na si kuwavua uanachama kama
ilivyojitokeza jambo ambalo lilipingwa na viongozi wa chama hicho,”
alisema Patrick.
Alisema,
kutokana na hali hiyo viongozi wa chama hicho akiwemo Mwenyekiti wake
Freeman Mbowe na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa alimwita na kumuambia
aache urafiki na Zitto la sivyo watamfukuza uanachama. (Walimwita lini,
wapi kwa namna gani, hivi kweli viongozi wa juu namna hiyo wanaweza
kumwita kiongozi wa wilaya hivi hivi tu, hicho chama si CHADEMA labda
CHAUMA na viongozi hao hawawezi kuwa Mbowe wala Slaa, lakini kibaya
kabisa, gazeti wala halikuwatafuta kutaka kujua upande wao na kupata
hata ukweli. Uandishi wa hatari sana huu)
“Waliniita
na kuniambia niachane na Zitto, nilipinga ndipo waliponiambia nijiondoe
ndani ya chama hicho, niliendelea kupinga,” alisema.
Alisema
kutokana na hali hiyo, viongozi hao walimwambia aitishe mkutano wa
Kamati ya Utendaji ya Wilaya na kuwaambia wajumbe wa kamati kuwa yeye si
rafiki wa Zitto na kwamba hawezi kumuunga mkono kwenye harakati zake,
lakini aliendelea kukataa suala hilo. (Hivi gazeti makini linaweza
kunukuu uongo kama huu na kusema limeandika habari kwa ajili ya watu
kusoma. Kuna tofauti gani na magazeti ya Yule jamaa mtunga hadithi).
“Tangu
nilipoitisha mkutano wa waandishi wa habari wa kupinga uamuzi wa
kuwavua uanachama akina Zitto, Mwigamba na Kitila, nimekuwa kwenye
mvutano mkubwa na viongozi wangu wa juu, nimepokea vitisho vingi ambavyo
nilivirekodi kwenye simu yangu ya mkononi waliyoichukua,” alisema
Patrick.
(Kwa
trend ambayo chanzo hicho kimeonesha tanguy huko juu, huna haja ya
kwenda hata darasa moja kujua kuwa huu ni uongo mkubwa unaosemwa na mtu
anayejifunza kuzalisha fitna na majungu, lakini pia mwanafunzi wa
kutengeneza mgogoro, lakini kikubwa kupika kesi. Mathalani mhariri
makini hawezi kupitisha uchafu kama huu uwe habari, angeuliza tu, huyo
Yona alifanya huo mkutano lini?, Ulihusu nini? Je ni kweli ulihusu
kupinga kuwavua uanachama watu hao? Kwa nini kutumika kuandika uongo?).
Aliongeza,
suala hilo liliendelea hadi Dk. Slaa na Mbowe walipomwita na
kumlazimisha aitishe tena kikao kingine cha kamati tendaji ili atangaze
kujiuzulu mwenyewe nafasi yake kabla ya kumfukuza uanachama, jambo
ambalo alilipinga tena. (Umakini wa waandishi na wahariri wa gazeti hilo
haukuwatuma kuona umuhimu wa kuwatafuta viongozi hao walau wahalalishe
huo uchafu walioamua kuuita ni habari ya kuwapelekea Watanzania. Hii ni
hatari sana.)
“Dk.
Slaa aliniandikia barua ya kunitaka niitishe mkutano nilipoona kelele
zinazidi nikaamua kuitisha lakini wajumbe wa kikao nilichoitisha kwa
pamoja wakaniunga mkono na kusema wana imani na mimi, hivyo basi
hawataki niondoke.
“Baada ya hapo, Dk. Slaa akaniandikia barua na kuniambia kuwa kikao nilichoitisha ni batili na kwamba wanatakiwa kuitisha kuitisha kikao kingine Januari 10 mwaka huu.”
Kwa
ujumla habari nzima ya Mtanzania ni crap. Na kuonesha dhahiri malengo
na nia ovu waliyonayo dhidi ya CHADEMA kupitia tukio hilo la kusikitisha
la kutekwa na kuteswa kwa Yona, gazeti hili ambalo limeandika mengi
sana ya KUUMIZA, yanayokiuka maadili na weledi wa uandishi, likimnukuu
mwenyekiti huyo akisema uongo dhidi ya Mbowe na Dk. Slaa, halikuwatafuta
viongozi hao, lakini likamtafuta Zitto Kabwe.
Wanaandika hivi;
“Nikiangalia
tukio langu na mgogoro uliopo ndani ya chama najua nimeumizwa kwa ajili
ya kumtetea Zitto, kwa sababu nimekuwa nikipokea vitisho kutoka kwa
viongozi wa juu wa chama na M4C,” alisema.
Kukamilisha
mpango huo wa spinning ya kuwahusisha viongozi wa CHADEMA na hatimaye
chama kizima katika sakata hilo, Zitto akatafutwa na akasema hivi;
Akizungumzia
tukio hilo, Zitto amesema vurugu kamwe siyo suluhu ya siasa nchini na
kwamba ni kitendo kinacholenga kuwaingiza watu katika woga na kuwatisha.
“Haya
ni matendo ya kikatili na ya kumuogopesha kutokana na kupinga baadhi ya
mapendekezo ya upande wa baadhi ya viongozi Kamati Kuu ya chama.
“Natoa
changamoto kwa viongozi zote wa Chadema kwamba sasa wakanushe kuwa
vurugu siyo silaha yao katika siasa,” alihitimisha Zitto.
Huyu
mtu tayari alishajua na kuhitimisha kuwa viongozi na chama chake
kinahusika na tukio hilo? Kwa nini anawahi kuhitimisha kuwasukumia tukio
zito kama hilo ambalo linaweza kuharibu kabisa chama chake ambacho eti
anataka kuwa mbunge na kiongozi wake. Au ni mwendelezo wa mkakati ule
ule, wakakutanishwa kwenye kipindi cha Star tv asubuhi yeye na Mwigulu,
Mwigulu Nchemba akajifanya anatoa habari ya ugaidi wa CHADEMA?
Habari
za kiuchambuzi juu ya mkakati huu wa kutaka kurudisha taswira ya ugaidi
na kuihusisha CHADEMA na matukio ya vurugu yanayohusisha umwagaji wa
damu ikipangwa kwa ustadi na wale wale, kwa mtindo ule ule, kwa malengo
yale yale, zitaongezwa baadae katika andiko hili;