MBUNGE WA MUSOMA VIJIJINI NIMROD MKONO AONGELEA JUU YASWALA LAKUMPA ZITTO KABWE MAGARI MAWILI.

Mbunge wa Musoma Vijijini - Nimrodi Mkono MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mb...

Mbunge wa Musoma Vijijini - Nimrodi Mkono

MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.


Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu kuwa aliwahi kumpa Zitto magari mawili.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.

“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.”

Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... “Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.

Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za kulikodisha...

“Hata nyaraka za umiliki wa gari hili ninazo mimi mwenyewe kama mmiliki halali. Ninamiliki magari mengi tu hata wewe mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu,” alisema Mkono.

Alisema wanafahamiana kwa siku nyingi hata kabla ya Zitto kuwa mbunge na kwamba aliwahi kufanya mazoezi kwa vitendo katika ofisi yake (Mkono), alipokuwa mwanafunzi.

Kuhusu tuhuma kwamba anawahonga wapinzani wake wajitoe katika uchaguzi ili apite bila kupingwa alisema katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000, 2005 na 2010 alipita bila kupingwa kutokana na uchapakazi wake wa kiwango kikubwa.

Mkono pia alijibu tuhuma zilizotolewa na Zitto jana kwamba Mbowe alipewa mamilioni ya fedha na Mkono kwa nyakati tofauti na kusema hajawahi kutoa fedha zozote kusaidia Chadema.

Zitto akana
Katika hatua nyingine, Zitto ameitaka Chadema kumwandikia mashtaka mapya yaliyoibuliwa na Lissu ili aweze kujitetea.
 
MWANANCHI

Related

OTHER NEWS 3005370117977571396

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item