NDOA YA OBAMA, MICHELLE SHAKANI
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya Ikulu ya Marekani, wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama alilazimika kushe...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/ndoa-ya-obama-michelle-shakani.html
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya ndani vya Ikulu ya Marekani,
wenza hao wamekuwa katika migogoro na Obama alilazimika kusherehekea
sherehe za mwaka mpya mjini Hawaii akiwa na binti zake wawili, Sasha na
Malia bila kuwepo Michelle.
Jarida la National Enquirer lilieleza kwamba katika moja ya matukio,
Obama aliwahi kukutwa akiwa na mwanamke mwingine katika ‘mazingira ya
kutatanisha’ wakati mkewe akiwa safarini.
Kutokana na ripoti iliyotolewa na Bombshel , Michelle na Obama wamekuwa
wakilala vyumba tofauti ndani ya Ikulu. Michelle pia anajiandaa kuhama
katika jumba lao pale Chicago ambalo wameishi wakati wa uchumba wao
miaka 21 iliyopita na kwa msisitizo watajadili juu ya talaka.
Taarifa ilidai tatizo limeanza miaka minane iliyopita pale Obama
alipodhamiria kujijenga kisasa. Ni mtoto wao Sasha ambaye aliumwa
ugonjwa unaosababishwa na woga wa maisha unaoitwa Spinal Meningitis
ndiyo uliowafanya waendelee kuwa pamoja.
Kitabu cha Anderson kinaelezea tatizo lilivyoanza baada ya Barack Obama
kuamua kuingia kwenye siasa, ambapo Michelle alisikika akimwambia
mumewe; “Wewe unajifikiria mwenyewe tu.”
Naye Barack Obama amesikika akisema: “Sikuwahi kufikiri kamwe kwamba
ningelea familia mwenyewe siku moja.” Anderson anadai kuwa Obama
amechoshwa na malalamishi ya mkewe.
“Nampenda sana Michelle lakini ananiumiza na ubishi wake wa kila mara,”
alisikika akisema Obama na kuongeza kuwa; “Anaonekana ni mwingi wa
machungu na hasira siku zote.”
Akizungumza na televisheni ya CBS ya Marekani, Anderson alidai kuwa
ilikuwa nusura Michelle atembee nje ya ndoa kwa sababu ya upweke.
Kwa miaka mitano wamekuwa na wasiwasi juu ya uwezo wao wa kupata watoto
kabla Malia hajazaliwa. Walishajadili sana suala la kuasilia watoto
(adoption) na marafiki zake wa karibu lakini kwa bahati nzuri Malia
alizaliwa mwaka 1998 na kuondoa wazo hilo.
Jina kamili la Obama ni Barack “Barry” Hussein Obama, Jr, alizaliwa
Agosti 4, 1961 Honolulu, Hawaii, alikulia huko huko Hawaii na Indonesia,
baba yake mzazi ana asili ya Kenya. Jina kamili la mkewe ni Michelle
LaVaughn Robinson, alizaliwa Januari 17, 1964 Chicago, Illinois.
Kukutana kwao
Barack na Michelle walikutana mwaka 1989 katika mazingira ya kikazi,
walifunga ndoa Oktoba 18, 1992, katika Kanisa la Umoja wa Kristu la
Trinity lililopo Chicago, Illinois.
Lakini vyanzo vingine vya taarifa zinadai kuwa ndoa haiko imara, hasa
baada ya tukio la Obama kupiga picha za pamoja bila aibu na Waziri Mkuu
wa Denmark, Helle Thorning-Schmidt (46) wakati wa mazishi ya aliyekuwa
rais wa kwanza wa Afrka Kusini, Neslon Madiba Mandela.
Obama akiwa na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron, alikuwa akicheka
na kumnong’oneza kitu waziri huyo mara kwa mara kwa muda wote, huku
Michelle akiwa pembeni yake amenuna. Mara nyingi alikuwa akimshika shika
mabega.
“Lakini kwa sasa Michelle anajiona kanyanyasika na kuaibishwa mbele ya
dunia kwani picha hizo zilirushwa duniani kote kupitia televisheni,
magazeti na mitandao mbalimbali. Alisikika akimtapikia Obama huku
akisema “Nimechoshwa.”
Pia tatizo limekuzwa na safari ya kikazi ya Obama hivi karibuni kule
Thailand ambayo ilimkutanisha na Waziri Mkuu mrembo kuliko pengine wote
duniani , Yingluck Shinawatra.
Tarifa zaidi zilieleza kwamba usalama wa taifa nchini humo unafahamu
kuhusu suala hilo, lakini umekuwa ukilichukulia kama suala binafsi na
Michelle alionekana kukasirishwa kupita kiasi alipopata taarifa hizo.
“Baada ya tukio hilo Michelle aliamua kuwasiliana na mwanasheria wake
akitaka kujua namna ya kuomba talaka na alimwambia Obama kwamba
anahitaji kuishi mbali naye,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Hata hivyo, kwa mujibu wa makubaliano waliyofikia, ilielezwa kwamba
Michelle ataendelea kuishi mjini Washington DC hadi binti yao mdogo,
Sasha (12) atakapomaliza elimu yake ya sekondari. Binti yao mkubwa,
Malia (15) tayari ameshaingia sekondari.
“Michelle (50) kwa sasa ataendelea kuishi kwenye Ikulu ya Washington
hadi Obama atakapomaliza muda wake wa urais ili tu aweze kuonekana kama
yupo, lakini aliweka wazi kabisa kwamba wataishi maisha tofauti,”
ilieleza ripoti hiyo ikimkariri mmoja wa vyanzo kutoka Ikulu hiyo.
Ripoti hiyo ilikariri chanzo hicho kikieleza; “Michelle kwa sasa anaishi
katika vyumba vya watumishi kwenye nyumba yao ya familia na anajiandaa
kuchukua vifaa vyake na kuvipeleka kwenye nyumba yao binafsi ya
Chicago”.
Taarifa nyingine ilieleza kwamba tayari mambo baina ya wanandoa hao
yameshakuwa magumu kiasi kwamba wamekuwa wakiishi kwenye vyumba tofauti
katika Ikulu ya Marekani.
Mgogoro wao
Barack na Michelle wamekuwa katika mgogoro kwa miaka kadhaa na
wanalazimika kuwepo pamoja kwa sababu tu ya watoto wao na kulinda hadhi
yake kisiasa. Lakini kwa sasa Michelle amekuwa mkali kweli kweli. Anaona
kama amepuuzwa na kudhalilishwa mbele ya dunia nzima na amekuwa akipiga
kelele akisema, “Nimevumilia vya kutosha”, taarifa zaidi zilieleza.
Kwa sasa Michelle anaonekana kupigania kukamilisha namna ya kupata
talaka, lakini baadhi ya taarifa zinaeleza kwamba anafanya makusudi
kuuchelewesha ili aweze kuukamilisha baada tu ya Obama kumalizia muda
wake wa urais ambapo ataweza kupata Dola za Marekani 30 milioni kupitia
mpango wa vitabu na zaidi ya dola 65 milioni kwa kuonekana hadharani.
“Kwa sasa Barack anaonekana kama amemwaibisha Michelle mbele ya dunia na
kwa hili ni wazi kwamba atalilipa kwa gharama kubwa,” kilieleza chanzo
kutoka Ikulu ya Marekani.
“Ni jambio lililo wazi kwa sasa kwamba Michelle ameshamwambia Obama
kwamba anahitaji kuishi mbali naye, japokuwa kwa sasa imekuwa ni suala
gumu kwa kuwa anahitaji aendelee kuonekana wakiwa pamoja kwa sababu
muhimu, lakini wanapokuwa nyumbani wanaishi maisha tofauti ya
kutengana,” kilieleza chanzo hicho.
Iwapo taarifa hizo ni sahihi, hii inamaanisha kwamba Michelle ameudhika
kupindukia na hii si mara ya kwanza jambo hilo kutokea miongoni mwao.
Tangu Obama alipochaguliwa kuwa rais, vitabu viwili vimemtaja vikidai
kwamba wenza hao walikaribia kutengana katika kipindi cha miaka yao ya
mwanzo ya ndoa na hata Michelle alifikia hatua ya kutaka kuomba talaka
akidai kwamba anaona maisha yake ya kisiasa yanawanyima furaha na kuwa
pamoja nyumbani.
Mwaka 2009 mwandishi wa siku nyingi wa Washington, Richard Wolffe
alisema kwamba ndoa hiyo ilikuwa sawa na iliyovunjika miaka tisa kabla
kutokana na harakati za kisiasa za Obama zilizokuwa zikimsababisha asiwe
karibu na familia kwa muda mrefu.
“Kulikuwa na mawasiliano kidogo sana na familia yake na hata mapenzi
yalipungua. Michelle alikasirishwa sana na hali hiyo akilaumu kwamba
mumewe anaonekana kuwa mbinafsi; ilimpa wakati mgumu sana,” aliandika
Wollfe.
Wakati huo Michelle alilazimika kutulia kwa kuwa tayari alishakuwa mama,
mbinti zao awili, Malia na Sasha kwa sasa wana miaka 15 na 12. Mumewe
ambaye walikutana kwa mara ya kwanza walipokuwa wakifanya kazi kwenye
shirika moja la sheria mjini Chicago mwaka 1989, alikuwa ndiyo kwanza
amechaguliwa kuwa Seneta wa Illinois na alikuwa akijipanga pia kuwania
nafasi kwenye baraza la Congress.
Mke wa Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, Carla Bruni
alipoulizwa katika moja ya vitabu kuhusu uzoefu wake wa maisha ndani ya
Ikulu alijibu, ‘Acha kabisa! Usiulize ni kama jehanamu. Sikuwahi
kuyafurahia’ ambapo Michelle alisema hakuwahi kuzungumza maneno ya aina
hiyo.
Mwaka 2012 mmoja wa waandishi wa masuala ya siasa, Edward Klein alieleza
kwamba Obama alionekana mwenye mawazo kupita kiasi, wakati ndoa yake
ilipokuwa kwenye matatizo mwaka 2000 kiasi kwamba rafiki zake walihofu
kwamba anaweza kujiua.
Alieleza kwamba Michelle alikuwa mwenye hasira kwa kuwa alimkataza Obama
kuwania nafasi kwenye Congress, ushauri ambao hakuufuata na hata hivyo
alishindwa kwenye uchaguzi. “Baada ya kushindwa alirejea kwa Michelle
kwa ajili ya kupata pumziko. Lakini Michelle hakuwa tayari kuonyesha
huruma yoyote,” aliandika Klein aliyedai kwamba marafiki wa Michelle
walimweleza kuwa tayari ameshafungua kesi akidai talaka.Chanzo Kwa
Msaada wa Mtandao wa CBS News