RATIBA YA MAZISHI YA ALIYEKUWA WAZIRI WA FEDHA MAREHEMU DK. WILLIAM MGIMWA

Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam KAMATI ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa...


Na Kiza Sungura- MAELEZO Dar es Salaam

KAMATI ya Taifa inayohusika na mazishi ya aliyekuwa waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa  imetoa ratiba ya mazishi ambapo mwili wa marehemu utawasili siku ya jumamosi tarehe nne saa saba mchana  katika uwanja wa Mwalimu Nyerere  Terminal  II na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni B jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Dk. William Lukuvi alisema kamati itakayohusika na mapokezi ya mwili wa marehemu ni ofisi ya Waziri Mkuu  itakayohusika na ndugu, viongozi na wananchi na Kamati ndogo ya mkoa wa Iringa inayoongozwa na mkuu wa mkoa huyo Dk. Christine Ishengoma.

Dk. Lukuvi alisema siku hiyo ya jumamosi saa kumi na moja jioni mwili marehemu utapelekwa katika hospitali ya Lugalo na tarehe tano siku ya jumapili saa tano na nusu asubuhi mwili wa marehemu utapelekwa katika  ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya ibada na kutoa heshima za mwisho.
Alisema ifikapo saa nane mchana mwili wa marehemu Dk. Mgimwa utapelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere Terminal I kwa ajili ya kuelekea Mkoa wa Iringa.

Ifikapo saa kumi kamili alasiri mwili wa marehemu utakuwa umewasili Mkoa wa Iringa katika uwanja wa ndege Nduli  na kuagwa na viongozi na wananchi wa mkoa huo katika ukumbi wa Siasa kilimo na baada ya hapo utapelekwa kijijini kwake Magunga.

Waziri Lukuvi alimalizia kwa kusema kuwa shughuli za mazishi ya Marehemu Dk. Mgimwa zitafanyika 6.1.2014 kuanzia majira ya saa sita mchana  katika kijiji cha Magunga mkoani Iringa na atazikwa kwa heshima zote za Kiserikali.

Related

TAARIFA KAMILI YA KIFO CHA MTOTO NASRA ALIYEISHI KATIKA BOKSI KISHA KUFARIKI DUNIA HOSPITALI YA MUHIMBILI DAR ES SALAAM YAIBUA SIMANZI NCHINI.

MSIBA wa mtoto Nasra Mvungi (4), aliyeteswa kwa kufungiwa katika boksi kwa zaidi ya miaka minne, ambako ndiko alikokuwa akipewa chakula, kwenda haja kubwa na ndogo na kulala, umeibua simanz...

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU DAR ES SALAAM (UDSM) AKUTWA AMEFARIKI BAADA YA KWENDA KUPUMZIKA HOSTEL

Mwanafunzi mmoja wa Kike wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam leo mchana muda wa saa nane amekutwa amefariki akiwa amelala kitandani chumba cha hostel, Inasemekana aliwaaga wenzake kuwa anakwen...

TASWIRA MBALIMBALI ZA MAZISHI YA MSANII RACHEL HAULE YALIYOFANYIKA JANA KATIKA MAKABURI YA KINONDONI

  Mchumba wa Marehemu Rachel, Saguda (katikati) akiwa na majonzi tele wakati wa mazishi ya mchumba wake  Majeneza yenye mwili wa marehemu Rachel na Mwanae yakiletwa Katika makab...

Post a Comment

emo-but-icon
:noprob:
:smile:
:shy:
:trope:
:sneered:
:happy:
:escort:
:rapt:
:love:
:heart:
:angry:
:hate:
:sad:
:sigh:
:disappointed:
:cry:
:fear:
:surprise:
:unbelieve:
:shit:
:like:
:dislike:
:clap:
:cuff:
:fist:
:ok:
:file:
:link:
:place:
:contact:


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904776
item