TAARIFA KUHUSU KIKAO CHA KAMATI KUU CHA CHADEMA KESHO
Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa ka...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/01/taarifa-kuhusu-kikao-cha-kamati-kuu-cha.html
Kutokana na maswali kutoka kwa wanahabari wa vyumba mbalimbali vya
habari juu ya agenda za kikao cha Kamati Kuu kesho, Chama kimetoa kauli
ifuatayo;
Ni kweli kutakuwa na mkutano maalum wa Kamati Kuu ya chama kesho
tarehe 3 Januari 2014 Jijini Dar Es Salaam. Ajenda kuu katika mkutano
huo ni tatu;
Mosi: Kupokea taarifa kuhusu mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba.
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Kamati Kuu itapokea taarifa juu ya kupitishwa kwa marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba 2013, kupitishwa kwa muswada wa kura ya maoni wa 2013, uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalum na kutolewa kwa Rasimu ya Katiba Mpya.
Pili: Kupokea utetezi (wa mdomo) wa wanachama watatu kuhusu tuhuma mbalimbali zilizoelekezwa kwao.
Wanachama hao walishajulishwa makosa yao kwa maandishi na
wamewasilisha utetezi wao wa maandishi. Wataitwa kwenye kikao kwa
kuzingatia matakwa ya kanuni 6.5.2 (b) na 6.5.2 (d) kupewa nafasi ya
kujitetea mbele ya kikao kinachohusika.
Tatu: Mpango Kazi wa Chama kwa mwaka 2014
Mpango Kazi wa chama ni sehemu ya hatua za utekelezaji wa Mpango
Mkakati wa Chama wenye dhima ya kuleta uongozi bora, sera sahihi,
mikakati makini na oganizesheni thabiti kwa maendeleo endelevu ya chama
na taifa.
John Mnyika
Mkurugenzi wa Mawasiliano