CCM YATEUA MGOMBEA WAKE UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KALENGA

      Dar es salaam. Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugomb...

 
  
Dar es salaam.
Kamati Kuu ya CCM, chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete, imempitisha Godfrey William Mgimwa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM, katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Machi 16, mwaka huu.

 Akizungumza na waandfishi wa habari jana katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, Kamati Kuu ya CCM  imemridhia Godfrey kupeperusha bendera ya CCM baada ya kukidhi vigezo licha ya kuongoza katika kura za maoni jimboni humo.

Godfrey ni Mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Kalenga na pia Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa ambaye ameliacha wazi jimbo hilo baada  kufariki dunia Januari 1, 2014.

 Pichani, Nape akimtambulisha Godfrey kwa waandishi wa habari, jana, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Related

TAARIFA YA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI KUHUSU BOMU LILILOLIPUKA ARUSHA

  Jumatatu July 07 kwenye moja ya migahawa iliyopo eneo la Uzunguni Jijini Arusha,Watu wanane waliripotiwa kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu.Mkurugenzi wa makosa ya jinai wa Jeshi la Poli...

NEWS ALERT: KITU KINACHOSADIKIWA NI BOMU CHALIPUKA ARUSHA‏ JIRANI NA MAHAKAMA KUU

Watu 7 wamejeruhiwa na 1 yuko mahututi baada ya watu wasiofahamika kurusha bomu karibu na Mahakama Kuu, Arusha  katika mgahawa wa Wama ulioko Gymkhana jijini Arusha(Pichani chini). Tukio ...

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI VITANDA 267 KWA SHULE ZA SEKONDARI JIMBONI KWAKE

 Mbunge wa Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimkabidhi vitanda Mkuu wa shule ya seondari ya Sekondari ya Mandera Bi. Rose Jumila, kushoto ni Diwania wa Viti maalum kata ya Msoga Bi. Maria ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904812
item