KATIBU MKUU WA UN AONYA KUHUSU GHASIA AFRIKA YA KATI (CAR)
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameonya kuwa ghasia zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, zinaweza kuligawa tai...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/katibu-mkuu-wa-un-aonya-kuhusu-ghasia.html
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ameonya
kuwa ghasia zinazoendelea katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, zinaweza
kuligawa taifa hilo na kuwatenga kabisa Wakristo na Waislamu.
Bwana Ban ameiomba Ufaransa kuwatuma wanajeshi
zaidi wa kutunza amani katika taifa hilo, ambalo limekumbwa na mapigano
ya kidini tangu mapinduzi ya kijeshi Machi mwaka uliopita.
Katika siku za hivi karibuni, maelfu ya Waislamu wamekimbilia nchi jirani, ili kuepuka mapigano hayo.
Katika ripoti mpya iliyochapishwa na shirika la
kutetea haki za kibinadam, la Amnesty International, inasema kuwa
wanajeshi wa Kimataifa wa kutunza amani nchini humo wameshindwa kuzuia
kile ilichokitaja kama mapigano ya kidini yanayodhamiria kuwaangamiza
raia wote ambao ni Waislamu.
Katika ripoti yake shirika hilo linasema kuwa
vikosi vya kimataifa vimesita kukabiliana na wanamgambo wa
AntiBalaka ambao wengi wao ni Wakristo wanaoendesha mashambulizi dhidi
ya Waislam.
Jamii nyingi za raia wanaoishi katika miji ya Kaskazini Magharibi mwa taifa hilo wameachwa bila ulinzi.