DKT. SHEIN ZIARANI NCHINI INDIA
STATE HOUSE ZANZIBAR OFFICE OF THE PRESS SECRETARY PRESS RELEASE Zanzibar ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/dkt-shein-ziarani-nchini-india.html
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 31 Januari, 2014
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
anaondoka nchini leo kuanza ziara ya siku tisa nchini India kufuatia
mwaliko wa Makamu wa Rais wa nchi hiyo Bwana Mohammad Hamid Ansari.
Akiwa
nchini humo Dk. Shein anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi hiyo na
jumuiya za wafanyabiashara kwa lengo la kukuza uhusiano kati ya Tanzania
na India pamoja na kuhimiza ushirikiano kati ya Zanzibar na India
katika nyanja za uchumi, biashara, uwekezaji, afya, kilimo na elimu.
Katika
ziara hiyo mbali na Mke wake Mama Mwanamwema, Dk. Shein amefuatana na
Waziri wa Fedha Omar Yusuf Mzee, Waziri wa Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii,
Vijana, Wanawake na Watoto Bibi Zainab Omar Mohamed, Waziri wa Biashara
na Viwanda na Masoko Nassor Ahmed Marzui na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Kimataifa Dk. Mahadhi Juma Maalim.
Wengine
katika msafara huo ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Mohamed Saleh Jidawi
na Katibu Mkuu Kilimo na Maliasili Affan Othman Maalim, Mshauri wa Rais
Ushirikiano wa Kimataifa, Uwekezaji na Uchumi Balozi Mohamed Ramia na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Zanzibar –ZIPA Salum Khamis
Nassor.
Akiwa
nchini India Jumapili tarehe 2 Februari, 2014 atatembelea Chuo cha
Barefoot kilichoko Tilonia ambako Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
inatarajiwa kusaini makubaliano ya ushirikiano na chuo hicho ambacho
kimejiegemeza katika kuwajengea uwezo kiuchumi, kijamii na kielimu
wanawake wazee na wajane waishio vijijini ili kuinua kiwango chao cha
maisha.
Siku
inayofuata tarehe 3 Februari, 2014 mapema asubuhi atazuru kumbukumbu ya
Mahatma Ghandhi ambako ataweka shada la maua na baadae atafanya
mazungumzo na Mwenyeji wake Makamu wa Rais.
Baadae
mchana siku hiyo atafanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa India Bwana
Manmohan Singh, ataonana na Waziri anayeshughulikia Diaspora na Waziri
wa Afya na Familia wa nchi hiyo. Jioni atakutana na watanzania wanaioshi
Delhi na baadae usiku atahudhuria chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa
heshma yake na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa India.
Tarehe
4 Februari, 2014 atatembelea kituo cha utafiti wa mazao ya kilimo,
atakutana na Jumuiya ya Wafanyabiashara na kuondoa kwenda mji wa
Hyderabad ambako siku inayofuata atakutana na Mwenyekiti wa hospiltali
za Appolo na kusaidia Makubaliano ya Ushirikiano.
Dk.
Shein siku hiyo atakutana pia na Baraza la Biashara ya Madawa Nchi za
Nje la India na baadae atapata fursa ya kutembelea kiwanda cha madawa
ambapo baadae atasafiri hadi mji wa Bangalore ambako siku ya Alhamisi
tarehe 6 Februari, 2014 atatembelea hospitali ya Manipal na kutia saini
makubalino ya ushirikiano na hospitali hiyo na baadae kuondoka kwenda
Mumbai.
Akiwa
Mumbai tarehe 7 Februari, 2014 Dk. Shein atatembelea Kampuni ya
kutengeneza matrekta ya Mahindra na baadae jioni atakutana na makampuni
ya biashara ya utalii na wakala wa safari za kitalii.
Jumamosi tarehe 8 Februari, 2014 Rais na ujumbe wake utatembelea kiwanda cha kusindika viungo (spices).
Rais
wa Zanzibar naMwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na ujumbe wake
utaondoka India Jumapili tarehe 9 Februari, 2014 kurejea nyumbani.