GRACE MVANDA KUWANIA UBUNGE JIMBO LA KALENGA IRINGA

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Grace Tendeya Mvanda, kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro c...

KAMATI Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimempitisha Grace Tendeya Mvanda, kuwa mgombea wake katika kinyang’anyiro cha ubunge katika jimbo la Kalenga, mkoani Iringa.

Grace Mvanda alikuwa mtu wa pili katika kinyang’anyiro cha kura za maoni jimboni humo. Aliyeshika nafasi ya kwanza alikuwa ni Lucas Sinkala Mwenda (31) ambaye Kamati Kuu haikupitisha jina lake.

Mwenda ni mhitimu wa Shahada ya Kwanza ya Sheria na sasa anataka kujiunga na Mafunzo ya Sheria kwa vitendo.

Uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga umepangwa kufanyika 16 Machi 2014. Uchaguzi huu unatokana na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Dk. William Mgimwa kufariki dunia miezi miwili iliyopita nchini Afrika Kusini.

Taarifa za ndani ya kikao zinasema, Kamati Kuu ilijadili kwa kina majina ya wagombea wote wa nafasi hiyo; huku wajumbe wakipata nafasi ya kuwahoji kila mgombea aliyekuwa anatafuta nafasi ya kupeperusha bendera ya chama.

Hatimaye Grace kwa kutumia ripoti za interejensia ya chama na vigezo vingine, aliteuliwa kuwakilisha chama katika kinyang’anyiro hicho.

Miongoni mwa vigezo vilivyotumika, ni kwamba mwanamama huyo aliwahi kugombea ubunge katika jimbo hilo mwaka 2005 kupitia chama cha Jahazi Asilia alishindwa.

Lakini alishika nafasi ya pili nyuma ya mgombea wa CCM. Taarifa zinasema, pamoja na kwamba JAHAZI Asilia hakikuwapo jimboni humo na mkoa wa Iringa kwa ujumla, lakini alifanikiwa kujinyakulia kura 13,500.

“Hii inaonyesha mgombea huyo anakubalika,” anaeleza Tundu Lissu, Mwanasheria mkuu wa chama hicho.

Lucas Sinkala Mwenda, alikubaliana kwa moyo mmoja na maamuzi ya Kamati na ameahidi kutoa ushirikiano kwa mgombea na kukisaidia chama chake kushinda.

Related

OTHER NEWS 2759407580063023614

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item