KAMATI KUU CCM YAWAHOJI WATATU JANA

  Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati...

 Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye akiwasili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma tayari kwa kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili.
 Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa akizungumza na Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye kabla ya kuanza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi Dodoma.
 Ndugu William Ngeleja akisubiri kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama.
Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Edward Lowasa kizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kuhojiwa na Kamati Ndogo ya Maadili kwenye Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi.



 DODOMA
Kamati Ndogo ya Maadili ya CCM inayoongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Phillip Mangula  jana imewahoji watu watatu ambao wawili walishawahi kuwa Mawaziri Wakuu katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania. Mawaziri hao waliohojiwa jana ni Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa, Waziri Mkuu wa Zamani Ndugu Fredrick Sumaye na Mbunge wa Sengerema Ndugu William Ngeleja ambaye pia alishawahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini.
 
 Kamati hiyo bado ina kazi ya kuwahoji viongozi wengine watatu ambao jana walishindwa kufika baada ya kuomba hudhuru kwani walikuwa na majukumu mengine ya kiserikali, ambao hawakuweza kuhojiwa jana ni Waziri wa Mambo ya Nje Ndugu Bernard Membe ambaye yupo safarini nje ya nchi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Ndugu Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia Ndugu Januari Makamba.

Related

WAHAMASISHAJI JAMII KUONGEZA NGUVU YA KAMPENI MPYA YA UZAZI WA MPANGO KIGOMA

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la World Lung Foundation Dk.Nguke Mwakatundu (katikati) akizungumza katika mkutano na Waandishi wa habari,waganga wakuu wa wilaya mkoani Kigoma na wahamasishaji jamii ku...

CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU TANZANIA(REDCROSS )KIMETOA MAFUNZO KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA MKOA WA MBEYA.

 Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba mwekundu (Redcross) Mkoa wa Mbeya, Ulimboka Mwakilili, akifungua mafunzo ya Redcross kwa Viongozi wa vyama vya siasa Mkoa wa Mbeya. Meneja wa Idara ya Ha...

MAMA SALMA AHUTUBIA MKUTANO WA WAKE WA MARAIS NA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA (OAFLA) NCHINI AFRIKA KUSINI

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akielekea kwenye ukumbi wa mkutano wa  Sandton Internationa Center unakofanyika mkutano wa wake wa Marais na  Wakuu wa Nchi za Afrika huko Johannesbu...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904754
item