MBUNGE AUAWA JAMHURI YA AFRIKA YA KATI
Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo, ameuawa kwa ...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/mbunge-auawa-jamhuri-ya-afrika-ya-kati.html
Mbunge mmoja wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambaye
alikuwa katika mstari wa mbele kupinga mauaji ya Waislamu nchini humo,
ameuawa kwa kupigwa risasi katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
Jean-Emmanuel Ndjaroua aliuawa na watu waliokuwa
wamejihami kwa bunduki waliokuwa wakitumia pikipiki, siku moja tu baada
ya kutoa hotuba kulaani mauaji yanayoendelea nchini humo.
Msemaji
wa shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, Peter
Bouckaert ameonya kuwa hali nchini humo inaendelea kuwa mbaya kila uchao
na raia wote wa nchi hiyo ambao ni Waislamu huenda wakalazimika
kutoroka katika kipindi cha wiki chache zijazo.
Maafisa wa kutoa misaada ya kibinadam wamesema
kuwa watu tisa wamefariki dunia kufuatia mapigano makali na uporaji
uliotokea katika mji mkuu jamuhuri ya afrika ya kati wikendi iliyopita.
Ripoti zinasema kuwa watu wawili wanaoaminika kuwa waislamu waliuawa kinyama wakati wa machafuko hayo.
Vita vikali vilitokea siku ya Jumamosi kati ya
wanamgambo wa Kikristo na Waislamu Magharibi mwa mji mkuu wa Bangui
ambapo majengo kadhaa yaliharibiwa kwa kuteketezwa.
Mapigano yaendelea katika sehemu kadhaa
Mkaazi mmoja wa Bangui alisema kuwa mtu mmoja
ambaye anatuhumiwa kumuua mama mmoja Mkristu aliuawa na mwili wake
kuchomwa na umati nje ya ukumbu wa baraza la mji huo.
Wanamgambo wengine wa Kikristu walimuua mtu Muumini mwengine wa
Kiislamu na wakati umati ulipokuwa ukijiandaa kuuteketeza mwili wake,
wanajeshi wa Rwanda, ambao ni sehemu ya kikosi cha jeshi la kutunza
ambani ya Muungano wa Afrika, MISA walifika mahala hapo na kumpiga
risasi.
Watu wengine watano waliuawawa kati hali isiyojulikana.
Peter Bouckaert wa shirika la kutetea haki za
kibinaadamu alithibitisha mauaji hayo na kuongeza kuwa mtu mwingine
aliuawa kinyama siku ya Jumapili karibu na soko kuu mjini Bangui.
Bwana Bouckaert alisema kuwa majeshi ya Rwanda
wamemueleza kuwa hali katika CAR inawakumbusha mauaji ya halaiki
iliyotokea nchini mwao miongo miwili iliyopita.
Jamuhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na mapigano
kwa karibu mwaka moja sasa tangu kundi la waasi la Seleka lilipomteua
Michel Djotodia kuwa rais wa kwanza Muislamu kufuatia mapinduzi ya
kijeshi mnamo machi mwaka wa elfu mbili kumi na tatu.
Mapigano hayo yameendelea hata baada ya Djotodia
kujiondoa na bunge kumuidhinisha Catherine Samba Panza kuwa kaimu rais
wa nchi hiyo mwezi uliopita na waislamu wamekuwa wakitoroka mapigano
hayo kwa maelfu.
Afisa huyo mwandamizi wa shirika la kutetea haki
za kibinaadamu ameiambia BBC kwamba baada ya siku au majuma machache
Waislamu wote wataihama Jamhuri ya Afrika ya Kati.
BBC