MBUNGE WA CCM JIMBO LA BAHI AKUMBWA NA KASHFA NZITO KATIKA MFUKO WA JIMBO MKOANI DODOMA

DODOMA.   MBUNGE wa Bahi (CCM), Omar Badwel ameingia katika kashfa baada ya Kamati ya Uhakiki wa Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimb...


DODOMA. 
MBUNGE wa Bahi (CCM), Omar Badwel ameingia katika kashfa baada ya Kamati ya Uhakiki wa Fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jimbo kubaini matumizi mabaya ya fedha hizo.

Kamati hiyo iliyoundwa na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, ilibaini kuwa fedha hizo zilitumika kinyume cha lengo la mfuko huo na pia taratibu za ununuzi hazikuzingatiwa.

Kuundwa kwa kamati hiyo yenye wajumbe watano, kulitokana na kuibuliwa kwa hoja ya ufisadi na Diwani wa Kata ya Lamaiti, Donald Mejitii mwishoni mwa mwaka jana.

Mejitii, ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa CCM Mko wa Dodoma alisema fedha hizo zilitolewa kwa ajili ya ununuzi na usambazaji wa majembe ya kukokotwa na ng’ombe.

Akizungumzia tuhuma hizo, Badwel alisema inawezekana kuwa kuna tatizo katika mfuko huo lakini akadai ripoti hiyo ina ukweli na uongo pia.

“Katika ripoti hiyo, sijaona sehemu ambayo mimi nilitoa majembe kwani katika mzunguko huu na mimi nilipeleka majembe 58 kwa ajili ya wananchi wangu. Nadhani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni,” alisema.

Akisoma taarifa ya kamati hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Bahi jana, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Julius Chitojo ambaye pia ni Diwani wa Zanka, alisema wamebaini wananchi wamedanganywa kwa kuuziwa majembe hayo kwa madai kuwa yana chapa ya Zimbabwe.

Pia, ilibaini kuwa majembe yaliuzwa kwa wananchi kwa Sh110,000 wakati makubaliano ya Kamati ya Mfuko wa Jimbo yalikuwa ni Sh85,000.

“Pia tumebaini kuwa makusanyo ya fedha kutokana na mauzo ya majembe hayo hayajarudi halmashauri ili wananchi walio wengi waweze kunufaika na mfuko huo wa jimbo badala yake fedha hizi zimechukuliwa na Said Kayumbo kwa maelekezo kuwa anampelekea Mbunge Badwel,” alidai Chitojo.

Chitojo alisema baadhi ya wananchi wamepata mgawo wa majembe ya bure wakati wengine wameuziwa na pia fedha za vikundi ziliingizwa katika akaunti ya Jumuiya ya Akiba na Maendeleo ya Bahi (Basada) kinyume na utaratibu.

Kuhusu madai hayo Badwel alisema alitoa orodha ya vijiji ambavyo alitoa majembe yaliyotolewa kwa mfuko wa jimbo na mengine ambayo sio ya mfuko lakini hayakuainishwa katika ripoti hiyo.

“Nilipoulizwa kuhusu fedha zilizotolewa kwa vikundi nilisema fedha zote zimetolewa na zimefika katika vikundi, nashangaa hapa kwenye taarifa haijaelezwa, vitu nilivyovisema havijatolewa, vitu vimepangwa na kamati,”
alisema Badwel.

MWANANCHI

Related

MTOTO ACHOMWA MOTO KISA SH. 500.

Mtoto Fatuma Hassan (9) anyedaiwa kufungiwa ndani kwa siku tatu kisha kuchomwa moto mikononi na mama yake mkubwa aliyetajwa kwa jina moja la Diana (38), mkazi wa maeneo ya Tandale.  Mam...

WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA 2014 AMBAO WALIMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2013 HAWA HAPA

Uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga Kidato cha Tano katika shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 umekamilika. Uchaguzi umefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya watahini...

WATUHUMIWA WAWILI WA UJAMBAZI BENKI YA NMB WAUAWA

Watuhumiwa wawili wa ujambazi wameuawa jijini Dar es Dalaam na wananchi katika jaribio la kufanya tukio la uporaji katika eneo la benki ya NMB Wilaya ya Ilala.Watuhumiwa hao wanadaiwa kuwa wa...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904812
item