TAARIFA YA TAHADHARI KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA   Simu: 255 22 2460735/2460706 FAKSI: 25...

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA UCHUKUZI
MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
 
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
  Unapojibu tafadhali nakili:Kumb. Na.: TMA/1622 10 Februari, 2014
 
Taarifa kwa Umma: Matarajio ya kuwa na Vipindi vya Mvua kubwa, Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa.
Taarifa Na.
201402-01
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 11 Jioni
Daraja la Taarifa:
Tahadhari
Kuanzia:
Tarehe
11 Februari, 2014
Mpaka:
Tarehe
13 Februari, 2014
 
Aina ya Tukio Linalotarajiwa
1. Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 ndani ya saa 24)
 
2. Hali ya Upepo mkali unaozidi kilomita 40 kwa saa pamoja na mawimbi makubwa zaidi ya mita 2.0
Kiwango cha uhakika:
Wastani (60%)
 
Maeneo yanayotarajiwa kuathirika
1. Vipindi vya Mvua Kubwa: Ukanda wa pwani mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba, Mbeya , Njombe, Ruvuma pamoja na kusini mwa mkoa wa Morogoro
 
2. Upepo Mkali na Mawimbi Makubwa: Pwani ya mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba
 
Maelezo:
Hali hii inatokana na kuwepo kwa kimbunga “FOBANE” kusini magharibi mwa Bahari ya Hindi. Mfumo huu unatarajiwa kuvuta upepo kutoka Pwani ya Somalia na misitu ya Congo kuelekea maeneo ya nchi yetu.
 
Angalizo:
Watumiaji wa bahari na wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada
Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo pale itakapobidi.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Related

MSOMI MKENYA PROFESA MAZRUI AFARIKI

Msomi mashuhuri wa Kenya,duniani Profesa Ali Mazrui ameaga dunia nchini Marekani. Mazrui alikuwa msomi wa maswala ya kisiasa, utamaduni wa kiafrika na maswala ya dini ya kiisilamu. Mazrui ...

KENYATTA AMKABIDHI MADARAKA RUTO

Kenyatta amemkabidhi mamlaka kwa muda naibu wake William Ruto kwa siku mbili atakazokuwa nje. Mahakama ya kimataifa ya ICC, inajianda kuwa mwenyeji wa mkutano maalum wa siku mbili kuhusu k...

SAMWEL SITTA: MAASKOFU NI UKAWA

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta sasa ‘ametangaza rasmi vita’ dhidi ya viongozi wa dini kwa kusisitiza kuwa hayuko tayari kuwaheshimu wala kuwavumilia ambao wanatoa nyaraka ...


LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

904822

HOT POSTSRECENTArchive

RECENT

Archive

item