TAZAMA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YALIYOJILI HUKO MKOANI MBEYA KWENYE MAADHIMISHO YA MIAKA 37 YA CCM
MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YALIFANYIKA JIJINI MBEYA Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili eneo la Soweto kuongoza mat...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/tazama-picha-za-matukio-mbalimbali.html
Mweneyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
akiwasili eneo la Soweto kuongoza matembezi ya mshikamano ya miaka 37
ya CCM, yaliyofanyika leo asubuhi mjini Mbeya.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitangaza kuwasili kwa Mwenyekiti wa CCM Rais Kikwete eneo la Soweto
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akipatiwa maelezo na Nape namna matembezi yatakavyoanza
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungiamikono wananchi kabla ya matembezi kuanza
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete akiwapungia mkono wananchi matembezi
yalipoanza eneo la Soweto. Wengine kushoto ni Katibu Mkuu wa CCM, Kinana
na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mbeya Godfrey Zamb
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi hayo huku
akiwa na watoto ambao aliwateua kutembea nao baada ya kuwaona eneo la
Soweto
SHEREHE ZIKAFANYIKA KWENYE VIWANJA VYA KUMBUKUMBU YA SOKOINE NA MWENYEKITI WA CCM AKAHUTUBIA WANA-CCM
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akiwasili katika Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya kuwaongoza wana-CCM katika kilele cha
maadhimisho ya miaka 37 ya CCM
Akiwapungia wananchi waliofurika katika Uwanja wa
Sokoine mjini Mbeya alipoingia Uwanjani
Hii ndiyo CCM, Rais Jakaya Kikwete akisema, huku akionyesha alama ya
CCM ya jembe na nyundo ambayo aliichukua kwa mmoja wa mashabiki wa CCM
walioingia nayo Uwanjani
Kikwete akizungumza kwenye kilele cha miaka 37 ya CCM
NA BASHIR NKOROMO, MBEYA
MWENYEKITI wa CCM, Rais
Jakaya Kikwete leo amevunja ukimya na kuzungumzia suala la mawaziri
waliotuhumiwa na wananchi kuwa mizigo wakati wa ziara za Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana na baadhi ya wajumbe wa sekretarieti katika
mikoa kadhaa nchini mwishoni mwa mwaka jana.
"Najua wapo baadhi ya watanzania,
walitaka
Mawaziri waliotajwa kuwa ni mizigo wafukuzwe kazi, na kwa vile
halikufanyika basi suala hilo limegeuzwa kuwa la malumbano,
ni vyema ieleweke kuwa kuitwa kwa Mawaziri hao na Kamati Kuu ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM), hakuna maana ya kuishia kufukuzwa", alisema,
Kikwete leo akihutubia maelfu ya watu katika sherehe za kilele cha miaka
37 ya CCM, kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Alisema
Mawaziri hao waliitwa kwa sababu ya kuwepo matatizo yaliyoonekana
yanatakiwa yapatiwe ufumbuzi, matatizo hayo yamezungumzwa na maelekezo
kutolewa kuhusu cha kufanya.
"Kamati
Kuu ya CCM imetimiza wajibu wake uliobaki ni wa serikali.Kamati Kuu
itaendelea kufuatilia na kama hakuna maendeleo ndipo inapoweza kuamua
kuomba mamlaka ya uteuzi ichukue hatua zipasazo dhidi ya mhusika.Huko
hatujafika" alisema Rais Kikwete.
Rais Kikwete alimpongeza
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akisema, ziara ambazo amekuwa
akifanya ni mfano unaopaswa kuigwa na viongozi wengine hasa wa CCM kwa
sababu ndio hasa unaotakiwa.
Alisema ziara za Kinana zinakijenga
Chama na kutoa taswira nzuri ya CCM katika jamii kwani zinahuisha uhai
wa CCM kwa kuwa Katibu Mkuu huyo katika ziara hizo huenda hadi kwa
wanachama waliopo ngazi za chini.
"Katibu
Mkuu Kinana amekuwa anafanya mambo ambayo baadhi ya watu wanadhani kuwa
ni mageni, lakini katika kufanya hayo amekuwa pia akionyesha umahiri na
ujasiri mkubwa kwa kwenda maeneo ambayo ni magumu kufikika" alisema
Rais
Kikwete na kuongeza;
"Katika ziara hizo
wakati mwingine amekuwa anatumia njia za usafiri zinazoogopesha,
amewahi kutumia meli ya MV Songea kutoka
mkoani Ruvuma hadi Mbeya, amepanda milima na mabonde kwa magari katika
maeneo ambayo ni hatari, lakini lengo likiwa ni kuhakikisha anawafikia
wanachama wa ngazi za chini kabisa".
Rais
Kikwete alisema mambo mengine yalivyomvutia katika ziara za Kinana, ni
hatua ya Katibu mkuu huyo kwenda kukaa na kula na wananchi katika ngazi
za chini na kisha kufanya nao kazi za maendeleo na zaidi kutoa fursa
kwa wananchi kueleza matatizo
na manung'uniko yanayowasibu.
Mwenyekiti
huyo wa CCM Taifa alisema Katibu mkuu wa Chama amekuwa anashiriki
katika kutafuta majawabu na matatizo anayoambiwa hali ambayo imesaidia
sana kumaliza baadhi ya matatizo kulekule mikoani.
"Pale
ambapo pamekuwa panahitaji hatua zaidi za serikali hakusita kutoa
taarifa kwa Waziri Mkuu, vile vile amekuwa anatoa taarifa ya ziara zake
kwenye Kamati Kuu ya CCM" alisema Rais Kikwete.