TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO MAALUMU YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA - SAYANSI NA HISABATI

TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO MAALUMU YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA MWAKA WA MASOMO 201...



TANGAZO LA NAFASI ZA MAFUNZO MAALUMU YA UALIMU TARAJALI NGAZI YA STASHAHADA KWA MASOMO YA SAYANSI NA HISABATI KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015

Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, anatangaza nafasi za Mafunzo Maalumu ya Ualimu Tarajali Ngazi ya Stashahada kwa masomo ya Sayansi na Hisabati. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo washiriki katika taaluma ya masomo mawili ya kufundishia katika shule za Sekondari. Mafunzo haya yatafanyika kwa utaratibu ufuatao:

(i)     Watakaochaguliwa watapatiwa mafunzo ya miezi mitatu ili kuimarisha taaluma ya masomo ya Sayansi na Hisabati waliyosoma katika Kidato cha Tano na cha Sita. Mwisho wa mafunzo haya, washiriki watafanya Mtihani Maalumu kwa lengo la kutathmini uwezo wao (competence) katika masomo tajwa.

(ii)    Watakaofaulu Mtihani wa mafunzo haya watajiunga na mafunzo ya ualimu ya kawaida Ngazi ya Stashahada kwa miaka miwili kuanzia mwezi Julai 2014. 

SIFA ZA WAOMBAJI

Waombaji wawe wamehitimu Kidato cha Sita kati ya mwaka 1998 na 2013 na kufaulu kwa kiwango kisichopungua ‘Subsidiary pass’ mbili katika tahasusi za PCB, PCM, PGM, CBG, CBA na CBN. 

MAELEKEZO MUHIMU

(i)     Waombaji wa mafunzo ya Ualimu watume maombi ofisi za Maafisaelimu wa Mikoa au Wilaya; au watume maombi yao kwa njia ya posta yakionesha anuani zao (za posta, au anuani ya barua pepe na simu); pamoja na nakala za vyeti vya ufaulu wa Kidato cha 4 na cha 6;

(ii)    Majibu kwa watakaochaguliwa kujiunga na mafunzo haya yatatolewa kwenye Tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz; OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz; na katika mbao za matangazo Wizarani, ofisi za Maafisaelimu wa Mikoa na Wilaya;

(iii)   Barua za kujiunga na mafunzo kwa watakaochaguliwa zitatolewa na vyuo watakavyopangwa kwa kutumia anuani zao; na

(iv)   Tangazo hili lipo pia katika tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi: www.moe.go.tz; OWM-TAMISEMI: www.pmoralg.go.tz na kwenye mbao za matangazo Wizarani, Maafisaelimu wa Mikoa au Wilaya; na Vyuo vya Ualimu.

Maombi yatumwe kwa anuani ifuatayo:

KATIBU MKUU,
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI,
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM       (Aione: Mkurugenzi, Idara ya Elimu ya Ualimu)

MWISHO WA KUPOKEA BARUA ZA MAOMBI NI TAREHE 28/02/2014.

Related

ELIMU 6617843665066990289

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item