UTALII UNAENDELEA DODOMA, SOMA HAPA ALICHOSEMA JULIUS MTATIRO KUHUSU BUNGE LA KATIBA
Ifikapo ijumaa tarehe 28/02/2014 inategemewa bunge la katiba litajadili na kuidhinisha rasimu ya kanuni za bunge maalum. Ijumaa tareh...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/02/utalii-unaendelea-dodoma-soma-hapa.html
Ifikapo ijumaa tarehe 28/02/2014 inategemewa bunge la katiba litajadili na kuidhinisha rasimu ya kanuni za bunge maalum.
Ijumaa tarehe 28 tayari wajumbe 639 tutakuwa tumelipwa jumla ya shilingi 300,000 x siku 12 x wajumbe 639 = 2,300,400,000/-(bilioni mbili milioni mia tatu na laki nne) au (milioni elfu mbili na mia tatu na laki nne).
La ajabu kuliko yote ni kuwa, wiki mbili zinakatika bila jambo lolote la maana kufanyika. Kambi za urais ndani ya CCM(Presidential Camps) zinapambana kufa na kupona kuhakikisha kambi mojawapo inatoa mwenyekiti wa bunge la katiba.
Kwa utafiti mdogo nilioufanya, ukamilishaji wa kanuni unapigwa danadana ili uchelewe kukamilika kutoa fursa kwa kambi iliyozidiwa kete ili wajipange katika kuusaka uenyekiti wa bunge la katiba.
Kambi ambayo inapigiwq chapuo na CCM ni ile ya Edward Lowassa ambayo mgombea uenyekiti wake ni mhe. Andrew Chenge.
Wakati CCM na Lowassa wanampigania kwa nguvu zote, upande wa pili yupo Samwel Sitta ambaye naye amejizatiti na amewagawa wabunge wa CCM na kuwafanya nusu wamuunge mkono Chenge(kwa kufuata msimamo wa chama) huku nusu wakimuunga mkono Samwel Sitta kutokana na utashi wao kwa kuzingatia rekodi walau ya kuridhisha aliyonayo hasa alipowahi kuwa spika wa bunge.
Rais Kikwete aliwahi kuahidi kuuacha mchakato wa katiba uwe huru, iweje tena leo chama chake kishinikize kwa nguvu nani awe mwenyekiti wa bunge la katiba? Na akishakuwa huyo wanayemtaka pana malengo kuwa aje kusimamia katiba ya watanzania au ya CCM?
Kwa vyovyote vile iwavyo, makundi ya urais ndani ya CCM yataliyumbisha sana bunge la katiba, "mark time" zitapigwa kila siku ili kambi inayopaswa kushinda ijipange, wajumbe tunaendelea kulipwa shilingi milioni 200 kwa ujumla kila kukicha ili kusubiri vita ya mafahali iishe.
Panahitajika mbinyo wa wananchi na sisi tuliomo humu bungeni kuwawakilisha wananchi, haiwezekani ati mchakato huru wa katiba ugeuzwe kuwa mapambano ya kambi za urais. Hili halikubaliki, siku ya ijumaa ikiwa wataleta DELAYS zao tutamweleza KIFICHO na wenzie kuwa tumechoshwa na KUKALISHWA DODOMA na kulipwa posho ambazo ni kodi za wananchi bila kazi.
Kila siku tunawaeleza wanaoyumbisha nchi hii ni CCM, pana watu wanatukejeli, nchi itamalizwa hii and "no body in power cares".