BIG RESULT NOW YAKUSANYA MABILIONI KATIKA KIPINDI CHA NUSU MWAKA
Msemaji Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina maalum kwa wanahabari, iliyofanyika katika Hoteli ya K...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/big-result-now-yakusanya-mabilioni.html
Msemaji
Mkuu wa Wizara ya Fedha, Ingiahedi Mduma, akizungumza wakati wa Semina
maalum kwa wanahabari, iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Park,
Misugusugu Kibaha, leo Machi 28, 2014. Semina hiyo imeandaliwa na Wizara
ya Fedha kwa lengo la utaratibu wa kutimiza utekelezaji wa Matokeo
Makubwa Sasa (Big Results Now).
KIBAHA.
Serikali
imekusanya jumla ya shilingi bilioni 215.0 katika kipindi cha Julai
hadi Disemba, 2013 kutokana na hatua mpya za kodi zilizoibuliwa kwenye
maabara za “Tekeleza kwa Matokeo Makubwa Sasa” yaani Big Results Now
(BRN), utaratibu unaotumiwa na Serikali katika kusimamia na kufuatilia
utekelezaji wa baadhi ya majukumu yake kwa lengo la kupata matokeo
makubwa kwa muda mfupi.
Haya
yamo katika taarifa aliyoitoa msemaji mkuu wa wizara ya Fedha Bi
alipokuwa akitoa taarifa ya utaratibu huo kwa wanablogu, katika kikao
maalum na wadau hao kilichofanyika nje kidogo ya mkoa wa Pwani, maeneo
ya Misugusugu.
Bi
Mduma alisema Wizara ya Fedha ni miongoni mwa Sekta zinazotekeleza
utaratibu huu hususan katika eneo la utafutaji wa mapato (Resource
mobilization), sekta nyingine ni Elimu, Kilimo, Maji, Uchukuzi na
Nishati.
Utekelezaji
wa kila sekta unazingatia viashiria vilivyoibuliwa katika uchambuzi wa
kimaabara ulioratibiwa na Serikali kwa kushirikiana na wataalam kutoka
nchini Malaysia.
Alisema
huu unaiwezesha Serikali kuongeza ufanisi katika kusimamia utekelezaji
wa majukumu yake ikiwemo usimamiaji wa miradi kwa kuweka wazi malengo
yaliyokusudiwa pamoja na kuainisha viashiria vya utekelezaji ili
kuongeza uwajibikaji kwa kila mshiriki.
Aidha,
viashiria hivi hutumika kupima hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa
maeneo ya kipaumbele na hivyo kuweza kupima mafanikio yaliyopatikana.
Kadhalika, utaratibu huu unasaidia kurekebisha mapungufu katika
utekelezaji kwa kuchukua hatua mapema na hivyo kuwezesha upatikanaji wa
matokeo makubwa kwa haraka.
Bi Mduma amesema wizara yake imedhamirisa utafuta mapato ya ziada kiasi cha shilingi trilioni 3.8 hadi kufikia mwaka 2015/16;