SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA MKUU WA MKOA WA MARA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JA...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/03/salamu-za-rambirambi-za-rais-kikwete.html
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho
Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Hawa A.
Ghasia kufuatia kifo cha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhe. John Gabriel Tuppa,
aliyefariki tarehe 25 Machi, 2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Pokea
rambirambi zangu za dhati na masikitiko makubwa kufuatia kifo cha
Mhe. John Gabriel Tuppa. Ni huzuni kubwa na pigo kwa Serikali na hasa
kwa Watendaji wenzake mkoani Mara ambao alikuwa akifanya nao kazi.
Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Marehemu John Gabriel Tuppa amefariki tarehe 25 Machi,2014 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Rais
pia amemwomba Mhe. Ghasia amfikishie salamu za pole kwa Mke wa
Marehemu,Watoto na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na kipenzi chao.
Rais amesema, anaelewa machungu wanayoyapitia katika kipindi hiki kigumu
kwani wamepoteza nguzo imara waliyokuwa wakiitegemea katika maisha yao.
“Hakika
tumempoteza kiongozi mchapakazi ambaye amekuwa akijituma na
kuwatumikia Wananchi wake hadi dakika za mwisho za uhai wake. Pengo
aliloliacha Marehemu Tupa haliwezi kuzibika kamwe lakini hatuna budi
kumwombea kwa Mwenyezi Mungu kuipumzisha roho ya Marehemu mahali pema
peponi” Amina.
Taratibu
na maandalizi ya mazishi zinafanywa kwa ushirikiano wa Familia, Ofisi
ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI.
Marehemu
Tupa alizaliwa tarehe 01 Januari, 1950 na katika enzi za uhai wake
amewahi kuongoza Wilaya za Chunya, Mwanga, Bukoba, Muleba na Dodoma
kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mwaka 2011. Ameacha Mke na
watoto watano.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
25 Machi,2014