MZEE WA MIAKA 61 AKATWA SEHEMU ZAKE ZA SIRI MBEYA
Majirani wakimuhudumia majeruhi ndani ya gari Gari ya wagonjwa toka Ileje ikiingia Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya. MBE...
https://gabriellabridalsolution.blogspot.com/2014/04/mzee-wa-miaka-61-akatwa-sehemu-zake-za.html
Majirani wakimuhudumia majeruhi ndani ya gari
Gari ya wagonjwa toka Ileje ikiingia Hospitali ya Rufaa mkoani Mbeya.
MBEYA
Katika hali
isiyokuwa ya kawaida mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la London
Haonga(61) mkazi wa Kijiji cha Mapogolo Kata ya Mbebe Wilaya ya Ileje
Mkoani Mbeya amejeruhiwa vibaya kwa kukatwa nyeti zake na watu watatu
wasiofahamika kisha kutokomea nazo kusikojulikana.
Tukio hilo
limetokea majira ya saa mbili usiku April 19 mwaka huu baada ya mmoja
kati ya watuhmiwa kufika nyumbani kwa mzee huyo kisha kubisha mlango
akiomba msaada wa kuonyeshwa njia akidai amepotea njia.
Mzee London
alipotoka nje ya nyumba akiwa anamwelekeza njia mtu huyo anayedaiwa
kuwani mjukukuu wake mita chache kutoka nyumbani kwake alifunikwa na
kitambaa usoni na watu wawili kisha kuangushwa na kukatwa nyeti zake
ambazo waliondoka nazo.
Mtendaji wa
Kijiji cha Mapogolo Cosmas Haonga amesema baada ya unyama huo Mzee
London alipoteza fahamu na alipozinduka alipiga yowe kuomba msaada
ambapo majirani walifika na kutoa msaada wa kumkimbiza Hospitali ya
Wilaya ya Ileje huku wakiwasaka watuhumiwa wa tukio hilo.
Kwa mujibu wa
Mtendaji wa Kijiji imedaiwa kuwa watuhumiwa wa tukio hilo wanatokea
Mpemba wilaya ya Momba ambao walitambuliwa na mhanga wa tukio hilo
ambapo baada ya kupewa PF 3 mzee London amekimbizwa Hospitali ya Rufaa
Mbeya ambapo alifikishwa Hospitali ya Rufaa majira ya saa 11:00 jioni
April 20 huku akilalamika kwa maumivu makali.
Kwa upande wake
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Ahmed Msangi amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kudai kuwa chanzo cha awali imedaiwa sababu za kutendewa
ukatili huo umetokana na mmoja wa ndugu aliyedai kuwa mzee huyo
anatuhumiwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mke wa mdogo wake hivyo
watu hao walitumwa kwa nia ya kulipiza kisasi.
Aidha imedaiwa
kuwa baadhi ya viungo vimekamatwa na wengine kudai kuwa tukio hilo
kuhusishwa na imani za kishirikina kwani imedaiwa watuhumiwa kuimbilia
nchi jirani mara baada ya kutenda kitendo hicho cha kikatili.
Kamanda Msangi
ameoa wito kwa jamii kuacha tabia za kujichukulia sheria mkononi amesema
pindi wanapokuwa na migogoro ni vema kutatua migogoro kwa njia ya
mazungumzo ili kuleta amani na kuahidi wale wote waliohusika na tukio
hili wanakamatwa na kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwani hakuna mtu
aliye juu ya sheria.
Chanzo: Mbeya Yetu