WANAFUNZI WATATU WAPOTEZA MAISHA WAKIOGELEA

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, linamshikilia mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama...

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Kinondoni, linamshikilia mfanyabiashara jijini Dar es Salaam, Mboka David (44) mkazi wa Kijitonyama kwa kosa la kusababisha vifo vya watoto watatu wa shule ya msingi na wengine saba kujeruhiwa walipokuwa wakiongelea katika bwawa la kuogelea ‘Swimming pool’ la Hoteli ya Landmark iliyopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam.
 
Taarifa za awali kuhusu tukio hilo ambalo lilitokea  Jumapili Aprili 27, mwaka huu saa 11 jioni katika hoteli hiyo zilidai mwanamke huyo ambaye sasa anahojiwa, aliwachukua watoto wake wakiwa na watoto wengine (wakiwemo waliokufa) kutoka majumbani mwao eneo la Kijitonyama karibu na Polisi – Mabatini bila ruhusa ya wazazi na kuelekea katika eneo hilo.
.
Habari  zaidi zinataarifu  kuwa, wakati wa tukio mama huyo akiwa na familia yake na watu wengine walikuwa wakijipatia kinywaji (pombe) ndipo watoto hao walipokuwa wakiogelea walizidiwa na maji na kupiga kelele ili kuomba msaada bila kupata mwitikio wowote na hata hapakuwa na mhudumu wa hoteli katika bwawa hilo huku wengine wakifanikiwa kujiokoa wenyewe.
 

Related

OTHER NEWS 2368139388735961707

Post a Comment

emo-but-icon

FOLLOW US

.

LISTEN / DOWNLOAD MUSIC HERE:

Total Pageviews

RECENT

Archive

item